Prussia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: yi:פרייסן
d roboti Nyongeza: hsb:Pruska; cosmetic changes
Mstari 1:
'''Prussia''' ni jina muhimu katika historia ya [[Ujerumani]] pia ya [[Poland]] na Ulaya wote. Katika [[karne ya 19]] hadi [[1933]] sehemu kubwa ya Ujerumani ilikuwa chini ya dola la Prussia lililokuwa awali nchi ya pekee na baadaye jimbo kubwa la Ujerumani.
 
== Nchi ya Waprussia ==
Kisasili lamaanisha nchi ya Waprussia waliokuwa kabila ya Kibalti kaskazini-mashariki ya Poland kwenye pwani za [[bahari ya Baltiki]]. Mnamo mwaka 1200 BK Waprussia walikuwa katika hali ya vita na Poland. [[Mwaka]] 1226 mtawala wa Poland aliomba usaidizi wa jeshi wa [[wamisalaba]] Wajerumani akiwaahidi mali katika maeneo watakaoteka baada ya kushinda Waprussia.
 
== Dola la Wamisalaba Wajerumani ==
Wamisalaba walifaulu kutekea eneo lilioitwa baadaya "Prussia ya mashariki" na kujenga himaya yao. Wamisalaba hawakuwa watemi wa kawaida bali wamonaki na wanajeshi. Dola la wamisalaba lilikuwa wakati mwingine chini ya mfalme wa Polandf, wakati mwingine dola la kujitegemea. Waliita walowezi na wakulima kutoka pande zote za Ujerumani na kuanzisha miji mingi.
[[ImagePicha:Ac.prussiamap2.gif|thumb|300px|<small>Brandenburg na Prussia kati ya 1600 na 1800 <br /> buluu nyeusi: Brandenburg asilia; Kijani nyeusi: nyongeza 1618 ya Prussia; kijani: nyongeza nyingine 1600 hadi 1772; njano: nyongeza kutokana na ugawaji wa Poland</small>]]
== Kuunganishwa na Brandenburg ==
Baada ya farakano kati ya Wakatoliki na Waprotestant himaya ya wamisalaba ilipokea uprotestanti na wamisalaba waliondoka katika maisha ya umonaki. Mkuu alikuwa mtemi mtawala akaoa.
 
Mkuu wa mwisho wa wamisalaba alikuwa mwana wa familia ya watemi wa [[Brandenburg]] katika [[Ujerumani]] hivyo Prussia imekuwa sehemu ya urithi wa familia hii iliyoendelea kutawala Prussia pamoja na maeneo yake ndani ya Ujerumani.
== Ufalme wa Prussia ==
1701 mtemi Friedrich wa Brandenburg alijiwekea taji ya Mfalme wa Prussia.
[[ImagePicha:Frederick II of Prussia Coloured drawing.png|thumb|left|200px|Friedrich II wa Prussia]]
Ufalme wa Prussia uliendelea kuwa muhimu kati ya madola ya Ujerumani. Watemi wa Brandenburg walirithi au kupata maeneo kwa njia ya vita hata katika magharibi ya Ujerumani. Mfalme [[Friedrich II wa Prussia]] alishindana na mataifa makubwa ya Ulaya katika [[vita ya miaka saba]] ([[1756]]-[[1763]]). Alikamata maeneo makubwa katika [[ugawaji wa Poland]].
 
Mstari 21:
Baada ya [[vita za Napoleoni]] mwanzo wa [[karne ya 19]] umuhimu wa Prussia uliendelea kukua.
 
== Prussia kama kiongozi wa Ujerumani ==
Katika ya vita ya wenyewe kwa wenyewe katika Ujerumani [[1866]] Prussia ilishinda Austria na kuwa dola kiongozi kati ya madola ya Ujerumani. Mwanasiasa mkuu wa nyakati zile alikuwa [[Otto von Bismarck]] kama [[waziri mkuu]] wa Prussia na baadaye kama [[chansella]] wa Ujerumani.
Baada ya kushinda [[Ufaransa]] katika vita ya 1871 sehemu zote za Ujerumani isipokuwa Austria ziliunganika chini ya uongozi wa Prussia na kuanzisha [[Dola la Ujerumani]]. Mfalme [[Wilhelm I wa Prussia]] alichaguliwa kuwa [[Kaisari]] wa Ujerumani. Alifuatwa na mtoto wake Friedrich III aliyekufa mapema halafu na [[Wilhelm II wa Ujerumani|Wilhelm II]]. Wakuu wale walitawala kwa cheo cha "Kaisari ya Ujerumani na mfalme wa Prussia".
[[ImagePicha:Deutsches Reich 1925 b.png|thumb|300px|Prussia (buluu nyeupe) ndani ya Ujerumani baada ya 1918]]
== Jamhuri ya Prussia ndani ya Ujerumani ==
Mwisho wa [[Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia]] ufalme wa Prussia kama vile katika sehemu zote za Ujerumani ilifutwa katika [[mapinduzi ya Ujerumani ya 1918]]. Wilhelm II akajiuzulu na kukimbilia Uholanzi. Prussia ilikuwa jimbo jamhuri ndani ya jamhuri la shirikisho la Dola ya Ujerumani.
 
Baada ya [[Adolf Hitler]] kuchukua utawala wa Ujerumani na kujenga [[udikteta]] madaraka ya majimbo yote pia ya Prussia yalifutwa.
 
== Mwisho wa Prussia ==
Mwaka 1945 mataifa washindi wa [[Vita Kuu ya Pili ya Dunia]] waliamua kutangaza mwisho wa Prussia wakiishtaki kuwa sababu ya tabia ya kivita ya Ujerumani. Maeneo ya Prussia yalifanywa kuwa majimbo katika Ujerumani kwa jumla. Prussia asilia yenyewe iligawiwa kati ya Poland na [[Urusi]], wakazi wake Wajerumani walifukuzwa.
 
[[CategoryJamii:Historia ya Ujerumani]]
 
[[CategoryJamii:Nchi ya Kihistoria ya Ulaya|U]]
[[Category:Historia ya Ujerumani]]
[[categoryJamii:Prussia]]
[[Category:Nchi ya Kihistoria ya Ulaya|U]]
[[category:Prussia]]
 
{{Link FA|nl}}
Line 68 ⟶ 67:
[[hi:प्रुशिया]]
[[hr:Pruska]]
[[hsb:Pruska]]
[[id:Prusia]]
[[io:Prusia]]