FORD-People : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 2:
 
==Chanzo katika FORD-Asili==
Chama cha ''[[Forum for the Restoration of Democracy]]'' ([[FORD]]) ndicho kilikuwa chama cha kwanza kujihusisha na harakati na mambo ya kisiasa tangu mwaka wa 1991, kwa kupigania kuruhusiwa kwa mfumo wa vyama vingi na demokrasia kutoka kwa [[mfumo wa chama kimoja]] na utawala wa [[KANU]] nchini Kenya. Rais [[Daniel arap Moi]] alishinikizwa na jamii ya kimataifa kuidhinisha mfumo wa vyama vingi kwa kubadilisha sehemu [[2A]] ya katiba ya Kenya, iliyozuia kuwepo kwa vyama vingi vya kisiasa.
 
Kabla ya uchaguzi wa 1992 [[FORD]] ilifarakana kati ya wafuasi wa viongozi [[Kenneth Matiba]] kutoka [[Mkoa wa Kati (Kenya)|Mkoa wa Kati]] na [[Martin Shikuku]] kutoka [[Mkoa wa Magharibi (Kenya)|Mkoa wa Magharibi]] kwa upande mmoja na kwa upande mwingine [[Jaramogi Oginga Odinga]] kutoka [[Mkoa wa Nyanza]]. Wafuasi wa [[Odinga]] waliunda [[FORD-Kenya]]. Wafuasi wa Matiba waliendelea kwa jina la [[FORD-Asili]].