Hamas : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 3:
 
Hamas ilianzishwa na Sheikh Ahmed Yassin, Abdel Aziz al-Rantisi na Mohammed Taha wa bawa la Misri la Undugu wa Kipalestina mwaka 1987 katika Intifada ya kwanza ya uasi dhidi ya utawala wa Israel katika nchi ya Palestina. Kupitia ufadhili wake na usimamizi wa shule, kliniki za afya ya huduma, misikiti, vikundi vya vijana, klabu za michezo, na vituo vya huduma ya siku, katikati ya miaka ya 1990 Hamas ilipata wafwasi wengi katika nchi ya Palestina. Inakadiriwa kuwa 80-90% ya mapato ya Hamas yanatumiwa katika kuendeleza afya, ustawi wa jamii, dini, utamaduni, na huduma za elimu. Katika pande za kijeshi Hamas ilihusika na washambuliaji wa kujiua dhidi ya Israel wa kwanza ukiwa 1993. Katika mwaka wa 2005 mashambuliaji ya kujiua yalisitishwa lakini yakaanza upya tena mwaka wa 2006. Katika miaka ya hivi karibuni Hamas ina hasa kushambulia Israel kwa roketi na moto chokaa.
 
Baada ya uchaguzi migogoro iliendelea kati ya Hamas na serikali ya Palestina, baada ya vita vya Gaza vya 2007 Hamas iliendelea kutawala Gaza na serikali ya Palestina iliwafukuza wabunge wa Hamas kutoka sehemu ya West Bank. Misri na Israeli zilifunga mipaka yake na Gaza na kuzuia kuingia na kutoka kwa watu na bidhaa. JUni 2008, Hamas ilisitisha mashambulizi yake ya roketi dhidi ya Israel baada ya makubaliano na Misri ya kusitisha mapigano.Licha ya makubaliano hayo mashirika mengine yaliendelea na mashambulizi dhidi ya Israeli. Miezi miwili kabla ya mwisho wa kusitisha mapigano ya miezi sita vita ilienea, baada ya wanajeshi wa Israeli kuwaua wapiganaji 7 wa Hamas katika mwezi wa Novemba 4.Mauaji haya yalianzisha upya mashambulizi ya roketi toka kwa Hamas. Israeli ilishambulia Gaza mwisho wa mwezi wa Desemba 2008. mashambulizi ya Israeli yaliendelea mpaka Januari 2009. Baada ya mashmabulizi hayo Israeli walifunga mipaka ya Gaza.