Bujumbura : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Badiliko: fy:Bûjûmbûra
CGN2010 (majadiliano | michango)
No edit summary
Mstari 20:
'''Bujumbura''', ni [[Mji Mkuu]] wa [[Burundi]] unaokadiriwa kuwa na idadi ya wakazi 300,000. Mji huu upo kaskazini mashariki mwa [[Ziwa Tanganyika]], na ni mji mkubwa zaidi Burundi, kitovu cha mawasiliano na uchumi nchini humo. Bujumbura ni mji pekee Burundi ambao una bandari ya kupakia mali na bidhaa mbalimbali za kuuza nje. Bidhaa kama [[kahawa]], [[pamba]], ngozi, na madini ya [[tini|stani]]. Kwa kijiographia Bujumbura iko 3°22'34" Kusini, 29°21'36" Mashariki (-3.3761111, 29.36) [http://earth-info.nga.mil/gns/html/cntry_files.html].
 
Bujumbura ilipanuka toka ilipokuwa kijiji kidogo kilichokuwa [[kambi ya Jeshi]] ya [[Wajerumani]]. Eneo hii iliitwa [[Afrika ya Mashariki ya UjerumaniKijerumani]] mwaka wa [[1889]]. Lakini, baada ya [[Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia]], Bujumbura ilichukuliwa na [[Wabelgiji|Ubeljiji]] ambapo [[Ligi ya Kimataifa]] ilisimamia [[Ruanda-Urundi]]. Jina la mji likabadilishwa kutoka '''Usumbura''' hadi Bujumbura Burundi ilipopata uhuru, mwaka wa [[1962]]. Bujumbura ni mji ambao umeshuhudia vita vya ukabila kati ya [[Wahutu]] na [[Watutsi]] kwa kung'ang'ania Uongozi wa Burundi.
 
Kati ya mji huu kuna majengo ni yale ya [[kikoloni]] na pia kuna [[soko]], [[uwanja wa taifa]], [[mskiti]] mkubwa na [[Kanisa|kathidro]]. Pia kuna [[Jumba la Makumbusho]] ambalo linaitwa jumba la makumbusho ya maisha na jumba la makumbusho ya Jiologia. Mambo mengine ya kuchangamsha ni kama [[Hifadhi ya Rusizi]], na [[Kiamba (Jiologia)|Kiamba]] hapo [[Mugere]], ambapo panasemekana kwamba [[David Livingstone]] na [[Henry Stanley]] walikutana. (Lakini watu wengi wasema walikutana [[Ujiji]]), [[Kigoma]], nchini [[Tanzania]] ambapo panasemekana ni [[mwanzo]] wa mto ulio unaosemekana kuwa hapo ndio mwanzo wa [[Mto Nile]].