Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Badiliko: hu:Nagy-hasadékvölgy; cosmetic changes
Mstari 2:
'''Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki''' ([[Kiing.]] '''Great Rift Valley''') ni maumbile ya kijiolojia inayoanza katika [[Mashariki ya Kati]] na kuendelea hadi [[Msumbiji]]. Ni kati ya maajabu makubwa ya dunia hii. Ufa hii imetokea tangu miaka milioni 35 kutokana na mwendo wa [[mabamba ya gandunia]] ya [[Bamba la Afrika|Afrika]] na [[Bamba la Uarabuni|Uarabuni]]. Mwendo huu umesababisha pia farakano ndani ya bamba la Afrika na wataalamu huamini kuwa Afrika ya Mashariki iko katika mwendo wa kuachana na Afrika kwa jumla.
 
== Uenezaji ==
[[Picha:Aerial jordan.jpg|thumb|200px|right|Bonde la [[mto Yordani]] ni sehemu ya ''Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki'']]
[[Picha:Great Rift Valley.png|thumb|200px|right|Mikono miwili ya Bonde la Ufa katika Afrika ya Mashariki]]
Mstari 8:
Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki lina urefu wa kilomita 6,000 kuanzia chanzo chake katika [[Syria]] hadi mwisho wake upande wa kusini katika [[Msumbiji]]. Upana wake ni kati ya kilomita 30 na zaidi ya 100; kina chake ni kati ya mita mia kadhaa hadi maelfu.
 
=== Sehemu ya Asia ya Magharibi ===
Upande wa kaskazini ufa inaanza kwenye mpaka wa [[Syria]] na [[Lebanoni]] ikionekana katika uwanja wa [[Beka'a]] kati ya [[milima ya Lebanoni]] na [[milima ya Lebanoni ndogo]].
 
Inaendelea katika mabonde ya [[mto Yordani]] na [[Wadi Araba]] hadi kuingia katika [[Ghuba ya Akaba]] na [[Bahari ya Shamu]].
 
=== Sehemu ya Uhabeshi ===
Ufa inaonekana tena upande wa Afrika kwenye [[Pembetatu ya Afar]] mpakani wa [[Eritrea]], [[Jibuti]] na [[Ethiopia]]. Hapa ufa imegawanyika. Mkono moja unaelekea mashariki-kaskazini katika [[Ghuba ya Aden]].
 
Mkono mkuu umepasua nyanda za juu za Ethiopia na nyanda za juu za Somalia ukielekea kusini. [[Mto Awash]] unafuata sehemu ya kaskazini ya bonde hili. Katika sehemu ya kusini kuna maziwa kama [[ziwa Abaya]].
 
=== Kugawanyika katika Kenya ===
Mpakani wa Ethiopia na Kenya bonde la ufa lajigawa kuwa na mikono miwili.
 
==== Mkono wa mashariki ====
Mkono wa mashariki unaonekana katika [[Ziwa Turkana]] na kuelekea kusini. Karibu na Nairobi unatokea kama bonde kubwa lenye kina kikubwa. Maziwa mengine ni maziwa kama Baringo, Bogoria, Elementaita, [[ziwa Nakuru|Nakuru]] na [[ziwa Naivasha|Naivasha]].
 
Mpakani na Tanzania kuna maziwa ya magadi kama Lake Natron. Ndani ya Tanzania baada ya kupita [[mlima Kilimanjaro]] bonde lapanuka hadi kutotambulika tena kwa macho. Kwenye [[uwanja wa Usangu]] linaonekana tena kama bonde lenye safu za milima kando. Mjini [[Mbeya]] mkono huu unakutana tena na mkono wa mashariki na kuendelea pamoja katika [[ziwa Nyasa]].
 
==== Mkono wa magharibi ====
Mkono wa magharibi huonekana vizuri kuanzia [[ziwa Albert]] na kuendelea katika maziwa ya [[ziwa Edward|Edward]], [[ziwa Kivu|Kivu]], [[ziwa Tanganyika|Tanganyika]] na [[ziwa Rukwa|Rukwa]]. Mbeya unakutana na mkono wa mashariki.
 
Kando la ufa kuna milima ya juu yenye asili ya ki[[volkeno]] kama vile safu za [[milima ya Virunga|Virunga]], [[milima ya Mitumba|Mitumba]] na [[milima ya Ruwenzori|Ruwenzori]].
 
=== Sehemu ya Kusini ===
Kusini ya Mbeya ufa inaendelea katika [[Ziwa Nyasa]] halafu katika mabonde ya [[mto Shire]] na sehemu ya mwisho wa [[mto Zambezi]] hadi kuingia katika [[Bahari Hindi]].
 
== Tazama pia ==
[[Bonde la Ufa]]
 
Mstari 66:
[[he:השבר הסורי-אפריקני]]
[[hr:Dolina velike rasjeline]]
[[hu:Nagy Hasadékvölgy-hasadékvölgy]]
[[id:Lembah Celah Besar]]
[[is:Sigdalurinn mikli]]