Kuku-mwamba : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa mpya
(Hakuna tofauti)

Pitio la 22:57, 7 Agosti 2010

Kuku-mwamba
Kuku-mwamba shingo-nyeupe
Kuku-mwamba shingo-nyeupe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Corvoidea (Ndege kama kunguru)
Familia: Picthartidae (Ndege walio na mnasaba na kuku-mwamba)
Jenasi: Picathartes
Lesson, 1828
Spishi: P. gymnocephalus (Temminck, 1825)

P. oreas Reichenow, 1899

Kuku-mwamba ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Picathartes, jenasi pekee ya familia Picathartidae. Wanatokea misitu ya Afrika chini ya Sahara. Kuku-mwamba wana domo kubwa kama lile la kunguru na kichwa bila manyoya chenye rangi kali (nyeusi na njano au nyekundu). Pia wana rangi ya nyeusi au kijivucheusi juu na nyeupe chini. Shingo yao ni nyeupe au ina rangi ya kijivu. Hula wadudu, kama bungo, mchwa na sisimizi, pia jongoo, tandu, nungunungu, konokono na hata vyura na mijusi. Hulijenga tago lao kwa matope chini ya mwamba. Jike huyataga mayai mawili.

Spishi