Solomoni : Tofauti kati ya masahihisho
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: ta:சுலைமான் நபி |
No edit summary |
||
Mstari 3:
'''Mfalme Solomoni''' kadiri ya [[Biblia]] alikuwa mfalme wa tatu na wa mwisho wa [[Israeli]] nzima, akitawala kuanzia [[970 K.K.]] hadi [[930 K.K.]] hivi.
Alikuwa mwana wa [[Daudi (Biblia)|Daudi]] na Bath-Sheba ([[Betsheba]]), aliyewahi kuwa [[mke]] wa [[Uria Mhiti]]. Daudi alimchagua kuwa mrithi wake kwa sababu alikuwa uthibitisho hai wa [[msamaha]] aliopewa na [[Mungu]] kwa [[kuzini]] na hatimaye kumuua Uria.
Ufalme wake ulitazamwa na [[Wayahudi]] kuwa na ustawi usio na mfano, kutokana na [[hekima]] yake na [[amani]] iliyopatikana wakati wote wa utawala wake.
Mstari 9:
Ufalme wake uliweza kustawi kuliko ule wa baba yake kutokana na msingi imara aliouweka Daudi. Lakini mwenyewe aliudhoofisha na kusababisha mara baada ya kifo chake utokee utengano kati ya makabila ya Kaskazini na yale ya Kusini.
Kati ya kazi muhimu alizozifanya, mojawapo ni kujenga [[hekalu la Yerusalemu]] na kuliweka wakfu kwa sherehe kubwa ya siku saba, ambapo Mungu alionyesha kibali chake kwa kulijaza kwa sura ya wingu ([[1Fal]] 8). Polepole [[hekalu]] hilo likaja kuwa la pekee hata [[patakatifu]] pengine pote pakakatazwa chini ya mfalme [[Yosia]].
Ingawa Solomoni anasifiwa kwa [[hekima]] yake, alishindwa kukwepa [[majivuno]] na [[tamaa]], akataka kuwapendeza wake zake waliokuwa 700 (mbali na masuria 300), wengi wao [[Wapagani]], hata akawajengea mahali pa kuabudia miungu yao akamchukiza Mungu hata akamtabiria mtoto wake atanyang’anywa sehemu kubwa ya ufalme (1Fal 11:1-13) ikawa hivyo.
Hata hivyo mwishoni aliweza kulaumiwa kwa kuzidisha fahari, hasa upande wa wanawake waliomvuta kwenda kinyume cha [[imani]] ya [[Mungu]] pekee.
Mstari 21:
[[Yesu]] alijitangaza kuwa mkuu na mwenye hekima kuliko Solomoni.
[[Jamii:Biblia]]▼
[[Jamii:Wafalme wa Israeli]]
▲[[Jamii:Watu wa Biblia]]
[[Jamii:Watu wa Kurani]]
[[Jamii:Manabii katika Uislamu]]
|