Chake Chake : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
New page: '''Chake Chake''' ni mji mkubwa kwenye kisiwa cha Pemba ambacho ni sehemu ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Maungano ya Tanzania. Ni makao makuu ya [[wilaya ya...
(Hakuna tofauti)

Pitio la 20:49, 1 Mei 2007

Chake Chake ni mji mkubwa kwenye kisiwa cha Pemba ambacho ni sehemu ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Maungano ya Tanzania. Ni makao makuu ya wilaya ya Chake Chake katika mkoa wa Pemba Kusini (South Pemba).

Katika kata tatu za Chachani, Tibirinzi na Wara kuna takriban wakazi 15,000.

Mji umeenea kwenye kilima juu ya hori inayoingia ndani ya kisiwa. Bandari ya Chake Chake haina kina cha kutosha kwa meli hivyo hutumiwa na jahazi au dau ndogo tu.

Kitovu cha mji ni eneo la sokoni penye maduka, hospitali, boma la kale na hoteli ya SMZ. Kando la mji kuna uwanja mpya wa michezo na hospitali mpya.

Uwanja wa ndege wa Wawi uko kilomita saba kutoka mjini upande wa mashariki. Huo ni uwanja wa ndege wa pekee kisiwani ukihudumia ndege ndogo tu.

Chake Chake inasemekana ni mji wa kale lakini hakuna majengo ya kihistoria ianyoonekana ila tu boma la kale. Habari zake zimepatikana tangu karne ya 19. Wataalamu huamini ya kwamba umeanzishwa tayari na Wareno karne 4 - 5 zilizopita kwa sababu minara yake yenye umbo la mraba si kawaida katika ujenzi wa Waswahili na Waarabu.

Chini ya mji kuelekea kihori kuna bado mabaki ya boma dogo penye mizinga miwili ya kale.