Tofauti kati ya marekesbisho "Chama cha Mapinduzi"

d
roboti Badiliko: en:Chama cha Mapinduzi; cosmetic changes
d (roboti Badiliko: en:Chama cha Mapinduzi; cosmetic changes)
'''Chama cha Mapinduzi''' (CCM) ni chama tawala nchini [[Tanzania]]. CCM ilizaliwa [[5 Februari]], [[1977]] baada ya kuungana kwa vyama vya [[Tanganyika African National Union]] (TANU) kilichokuwa kikitawala Tanzania Bara na [[Afro-Shirazi Party]] (ASP) kilichokuwa chama tawala cha [[Zanzibar]] wakati huo. Chama cha Mapinduzi kilikuwa kikiongozwa na [[Mwalimu Nyerere]] na Afro-Shiraz Party kilikuwa chini ya [[Amaan Karume]].
 
== Itikadi ==
Kwa miaka mingi CCM ilikuwa ikifuata siasa ya [[Ujamaa na Kujitegemea]]. Itikadi hii ilipewa nguvu za kisera mwaka 1967 lilipotangazwa [[Azimio la Arusha]]. Kutokana na azimio hilo uchumi uliwekwa mikononi mwa umma. Itikadi hii pia ilisisitiza umuhimu wa kuishi pamoja hasa katika vijiji vya Ujamaa.
 
== Uchaguzi ==
CCM imekuwa ikishinda chaguzi za Urais toka mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa nchini Tanzania. Chama hicho kimekuwa pia kikipata idadi kubwa ya wabunge wa [[Bunge la Muungano]] na [[Baraza la Wawakilishi]]. Chaguzi za vyama vingi Tanzania baada ya kurejeshwa kwa mfumo huo zilifanyika mwaka 1995, 2000, na 2005.
 
== Uongozi ==
Katika historia ya CCM kumekuwa na wenyeviti wanne:
* [[Julius Nyerere]], 1977 - 1990,
* [[Ali Hassan Mwinyi]] 1990 - 1996
* [[Benjamin Mkapa]] 1995 - 2005,
* [[Jakaya Kikwete]] 2006 -
 
== Viungo vya nje ==
* [http://www.ccmtz.org/ Tovuti ya Chama cha Mapinduzi]
 
[[CategoryJamii:Siasa ya Tanzania]]
 
[[de:Chama Cha Mapinduzi]]
[[en:Chama Chacha Mapinduzi]]
[[fi:Chama Cha Mapinduzi]]
[[it:Partito della Rivoluzione]]
44,101

edits