Hanse : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: simple:Hanseatic League
No edit summary
Mstari 3:
'''Hanse''' ([[Kijerumani]]:die Hanse, [[Kiholanzi]]: de Hanze,[[Kisweden]]: Hansan) ilikuwa shirikisho la miji ya biashara katika Ulaya ya Kaskazini na hasa ushirikiano wa wafanyabiashara wa miji hii.
 
==Ushirikiano wa kusaidiana==
Ushirikiano huu ulikuwa mwanzoni na shabaha ya kusaidiana katika ulinzi wa njia za biashara dhidi ya [[majambazi]] na [[maharamia]]. Wanfanyabiashara wa Hanse waliendelea kupeana msaada pia katika mambo ya biashara yenyewe kwa kupunguza mashindano kati yao wenyewe na dhidi ya biashara isiyokuwa ya Hanse.
 
==Kilele cha Hanse==
Kati karne ya 13 hadi 16 shirikisho la Hanse ilikuwa na nguvu kubwa ya kiuchumi, kisiasa na kijeshi. Msingi wa uwezo wake ulikuwa biashara yenye faida kubwa katika [[Bahari ya Baltiki]]. Malighafi kutoka [[Urusi]] ya Kaskazini na [[Skandinavia]] kama vile [[ngano]], [[ubao]], [[nta]] na [[ngozi ya manyoya]] zilipelekwa Ulaya ya Kati wakati bidhaa kutoka miji ya Ulaya ziliuzwa kwa faida nzuri. Wafanyabiashara wa Hanse walitawala kabisa biashara kwenye Bahari ya Baltiki hawakuruhusu wengine kuingia hapa. Mji wa [[Novgorod]] ulikuwa kituo muhimu cha Hanse katika Urusi.
 
Kitovu cha Hanse kilikuwa miji ya Ujerumani ya Kaskazini kama vile [[Lübeck]], [[Hamburg]] na [[Danzig]]. Miji ya Hanse ilikuwa pia na maeneo ya ghala maalumu hadi [[London]] na [[Uholanzi]]. Wawakilishi wa miji ya Hanse walikutana katika mikutano na kuamua juu ya siasa ya pamoja. Wakati wa karne ya 14 manowari na wanajeshi wa Hanse ziliweza kumshinda hata mfalme wa [[Denmark]] aliyelazimishwa kukubali kipaumbele cha Hanse katika Baltiki.
 
==Kurudi nyuma tangu karne ya 16==
Tangu karne ya 15 uwezo wa Hanse ulianza kupungua kwa sababu watawala makabaila wa bara walipanusha maeneo yao. Novgorod iliharibika vitani na kuwa sehemu ya utemi wa [[Moskva]]. Miji midogo zaidi ya Hanse ililazimishwa kukubali ukuu wa watawala jirani. Kwa hiyo nguvu ya ushirikiano wa Hanse kwa jumla lipungua polepole. [[Vita ya miaka 30]] (1618-1648) katika Ujerumani iliharibu Hanse ya awali kabisa. Miji iliyobaki ilikutana mara ya mwisho mwaka 1669 lakini nguvu ya zamani haikuweza kurudishwa.