Tofauti kati ya marekesbisho "Ekaristi"

42 bytes added ,  miaka 9 iliyopita
d
roboti Nyongeza: hy:Հաղորդություն; cosmetic changes
d (roboti Nyongeza: tr:Efkaristiya gizemi)
d (roboti Nyongeza: hy:Հաղորդություն; cosmetic changes)
Kwa [[Ukristo|Wakristo]] '''Ekaristi''' ni [[sakramenti]] iliyowekwa na [[Yesu Kristo]] wakati wa [[karamu ya mwisho]] usiku wa kuamkia [[Ijumaa Kuu]], siku ya mateso na kifo chake.
 
== Jina ==
[[ImagePicha:01preparation4.jpg|thumb|200 px|right|Vipaji vya [[mkate]] na [[divai]] vilivyoandaliwa kwa [[adhimisho]] la ekaristi.]]
 
Jina linatokana na neno la lugha ya [[Kigiriki]] εὐχαρίστω (''eukharisto'': nashukuru) lililotumiwa na [[Mtume Paulo]] na [[Wainjili]] katika kusimulia karamu hiyo ya mwisho ya [[Yesu]] na [[Mitume wa Yesu|Mitume]] wake, na muujiza uliotangulia ambao Yesu alidokeza nia yake ya kushibisha [[binadamu]] wote, yaani ule wa kuzidisha mkate na samaki kwa ajili ya umati.
Shukrani ilikuwa msimamo wa msingi wa Yesu kwa Baba maisha yake yote, hasa alipofikia wakati wa kutolewa awe kafara ya wokovu wetu. “Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, ‘Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu’. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, ‘Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu’” (1Kor 11:23-25).
 
== Mkate na divai ==
 
Yesu alitumia mkate na divai kwa sababu vilikuwa vya maana sana katika utamaduni wake na katika Agano la Kale. Vilikuwa chakula cha kawaida na kinywaji cha karamu. “Divai imfurahishe mtu moyo wake... na mkate umburudishe mtu moyo wake” (Zab 104:15). Vilitokana na chembe za ngano na matunda ya mzabibu ambavyo Yesu alijifananisha navyo. “Amin, amin, nawaambia: Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi” (Yoh 12:24). “Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote” (Yoh 15:5). Baada ya kulimwa, vilihitaji kusagwa au kushinikizwa, matendo yanayodokeza tena mateso yake pamoja na kazi ya binadamu. Pia wingi wa chembe na wa zabibu zinazoungana ziwe mkate na divai unamaanisha umoja wa waamini ndani ya Kristo. Kwa hiyo ni lazima tutumie daima mkate na divai, si vitu vingine.
Hatimaye Yesu alitumia divai kuachia ishara ya damu yake ili wafuasi wake waweze kushiriki mateso yake. “Je, mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi?” (Math 20:22). Kisha kushiriki kila mwaka karamu ya Pasaka, ambapo wote walikunywa divai mara nne, safari ya mwisho alikamilisha miujiza yake kwa kuigeuza iwe damu yake. “‘Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu’. Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, ‘Twaeni hiki, mgawanywe ninyi kwa ninyi; maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja’. Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, ‘Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu’. Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula, akisema, ‘Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu’” (Lk 22:15-20). “Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je, si ushirika wa damu ya Kristo?” (1Kor 10:16).
 
== Ushuhuda wa [[Biblia]] ==
 
[[Agano Jipya]] linasimulia mara nne matendo na maneno ya Yesu ambayo alianzisha ibada hiyo na kuwakabidhi Mitume wake.
Simulizi la zamani zaidi ni lile la [[Barua ya kwanza kwa Wakorintho|1Kor]] 11:23-25. Likafuata lile la [[Injili ya Marko|Mk]] 14:22-24; halafu yale ya [[Injili ya Mathayo|Math]] 26:26-28 na [[Injili ya Luka|Lk]] 22:19-20.
 
== Asili ==
 
Kadiri ya ushuhuda huo, Yesu, katika karamu ya mwisho aliwagawia mitume wake mkate na divai akisema ndio mwili wake na damu yake vitakavyotolewa kama [[kafara]] kwa ondoleo la [[dhambi]] za umati, akawaagaiza wafanye vilevile kwa [[ukumbusho]] wake.
Simulizi la Paulo linafanana na lile la [[Mwinjili Luka]] na kufuata jinsi ekaristi ilivyoadhimishwa kati ya Wakristo wa mataifa; kumbe [[Mwinjili Marko]] na [[Mwinjili Mathayo]] waliripoti adhimisho lilivyokuwa kati ya Wakristo wa Kiyahudi.
 
== Maendeleo ==
 
[[ImagePicha:BentoXVI-51-11052007.jpg|thumb|left|360px|[[Papa Benedikto XVI]] akiadhimisha ekaristi]]
Karne zilizofuata ibada ilizidi kubadilika, hasa ilipotenganishwa na mlo wa kawaida ulioendana nayo awali. Badala ya mlo huo, ibada iliunganishwa na masomo ya [[Neno la Mungu]].
 
Kati ya namna mbalimbali za kuiadhimishwa, yalijitokeza mapokeo ya mashariki na ya magharibi. Kwa jumla mapokeo ya mashariki yanahusisha milango ya fahamu na ni ya fahari kuliko yale ya magharibi.
 
== Teolojia ==
 
Ekaristi inahusiana sana na [[Pasaka]], na [[kifo]] na [[ufufuko]] wa [[Yesu]] vilivyotokea kwenye sikukuu hiyo ya [[Wayahudi]].
 
 
== Katika mpangilio wa sakramenti saba ==
 
Katika imani ya [[Kanisa Katoliki]] na [[Waorthodoksi]] sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ekaristi, iliyo kuu kuliko sakramenti zote kwa sababu ndiyo Yesu mzima, Mungu-mtu, katika maumbo ya mkate na divai. Walioshiriki kifumbo kifo na ufufuko wake wakapokea kwake paji la Roho Mtakatifu, wanaalikwa kukaribia mara kwa mara meza anapowalisha na kuwanywesha Mwili na Damu yake ili washiriki uhai wake kwa dhati zaidi na zaidi. “Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi” (Yoh 6:56-57). Ubatizo na kipaimara havirudiwi, vinadumu ndani ya mtu kama mifupa ambayo ekaristi ya mara kwa mara inazidi kuitia mwili na damu.
 
[[CategoryJamii:Liturujia]]
[[CategoryJamii:Sakramenti]]
 
[[ar:إفخارستيا]]
[[hr:Euharistija]]
[[hu:Eucharisztia]]
[[hy:Հաղորդություն]]
[[ia:Eucharistia]]
[[id:Perjamuan Kudus]]
43,953

edits