Fumbwe : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa mpya
 
dNo edit summary
Mstari 33:
''[[Vidua wilsoni|V. wilsoni]]'' <small>([[Ernst Hartert|Hartert]], 1901)</small>
}}
'''Fumbwe''' ni [[ndege (mnyama)|ndege]] wadogo wa [[jenasi]] ''[[Vidua]]'' katika [[familia (biolojia)|familia]] [[Viduidae]] ambao wanatokea [[Afrika]] tu. [[Spishi]] bila mkia mrefu na yenye rangi ya [[nili]] wanaitwa [[kinili]] pia. Wakati wa kuzaa madume wana rangi ya nyeusi na nyeupe na pengine rangi nyingine au rangi ya nili tu, na spishi kadhaa zina mkia mrefu. Lakini wakati wengine wana rangi za majike, kahawia na nyeupe, wenye michirizi miwili kwa utosi, na mkia wao una urefu wa kawaida. Hula [[mbegu]] za [[nyasi|manyasi]] hasa lakini [[mdudu|wadudu]] pia, [[kumbikumbi]] aghalabu.
 
Ndege hawa hawajengi tago lao lenyewe lakini huyataga [[yai|mayai]] yao katika matago ya ndege wa familia [[Estrildidae]] ([[udusio wa kiota]], Kiing. [[w:Brood parasitism|brood parasitism]]). Kila [[spishi]] inadusia spishi yake ya Estrildidae. Vinili wadusia [[mtolondo|mitolondo]], [[mshigi tombo]] au [[mshigi kidari-machungwa]], na fumbwe wengine wadusia [[tunguridi]], [[tunguhina]] au [[mshigi|mishigi]] mbalimbali. Kinyume na [[kekeo]] fumbwe hawaharibu mayai ya mwenye tago. Huyataga mayai 2-4 kwa kuzidi yaliyomo. Mayai ya fumbwe ni meupe kama yale ya mwenyeji lakini wakubwa zaidi. Ndani ya domo la makinda inafanana na ile ya makinda ya mwenyeji na dume anaiga wimbo wake.