Jina la mkoa ([[Mkoa wa Mbeya]]), wilaya na mji wa [[Tanzania]] Kusini-Magharibi
== Mkoa wa Mbeya ==
Mkoa wa Mbeya imepakana na [[Zambia]] na [[Malawi]], halafu na mikoa ya Rukwa, Tabora, Singida na Iringa. Kuna wilaya zifuatazo: Mbeya mjini, Mbeya vijijini, Rungwe, Mbozi, Chunya na Chimala. Mbeya ni kati ya maeneo yanayopendeza kabisa ndani ya Tanzania ikiwa na sehemu za [[Ziwa la Nyasa]], [[Ziwa Rukwa]], [[Milima ya Mbeya]], [[Milima ya Rungwe]], Uwanja wa juu wa Uporoto, Uwanja wa Usangu ingawa haukufikiwa na utalii.
Wilaya ya Rungwe ni eneo penye mvua nyingi katika Tanzania. Mkoa wa ujumla ni mojawapo kati ya mikoa yenye kilimo kizuri inayotoa mazao ya kulisha taifa. Lakini maeneo makubwa ya Wilaya ya Chunya ni makavu.
Wilaya ya Chunya ina madini mbalimbali hasa dhahabu.
Mbeya na Mbozi kahawa hupandwa. Rungwe pana chai nyingi, pamoja na Rungwe na Chimala hulimwa mpunga. Nyanda za juu kuna nafaka na viazi.cocoa.