Nishati : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
New page: '''Nishati''' ==Ufafanuzi== Ni nguvu iwezeshayo kazi kufanyika. Kazi, kifizikia; ni kitendo kinachohusisha mabadilishano ya namna moja ya nishati hadi ingine ama pia kubadili hali ya...
(Hakuna tofauti)

Pitio la 11:34, 15 Juni 2007

Nishati


Ufafanuzi

Ni nguvu iwezeshayo kazi kufanyika.


Kazi, kifizikia; ni kitendo kinachohusisha mabadilishano ya namna moja ya nishati hadi ingine ama pia kubadili hali ya kimaumbile na nafasi. Kwa mfano, kusogeza kiti ni kazi inayojidhirisha kwa kuhamisha kiti toka nukta moja hadi ingine.

Kizio cha kazi ni Juli.


Thathmini ya kihesabu ya kazi kulingana na nishati kifizikia hukokotolewa kwa thamani ya Juli na kadhaa.


Hali Kuu Mbili


Hujidhihirisha katika sura mbili na kutathminiwa hivi:


  • Nishati Uweza
  • Nishati Mwendeko


Nishati Uweza


Hii ni hali ya kiutathmini uwezo wa nishati kufanya kazi ama kuleta zao fulani la kikazi katika wakati ambao tukio halisi halijatendeka. K.m. jiwe juu ya kigingi cha mlima kabla halijadondoka lina tathmini ya uwezo wa nguvukazi sawa na mara litakapofika chini wakati wa kudondoka.


Nishati Mwendeko


Hii ni hali ya kiutathmini uwezo wa nishati kufanya kazi endelevu kiwakati. K.m. Jiwe lililorushwa lina nguvukazi alhali likipea.


Aina Za Nishati

Hutokana na asili au chanzo chake. Zifuatazo ni Baadhi yake:-



Makundi ya Nishati

Nishati kuwekwa katika makundi kulingana na matumizi ya mwanadamu na ukubwa wa uhitaji wake katika sura ya kijamii halafu pia na aina ya matumizi.