Kishawishi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|[[Adamu na Eva wakishawishiwa katika bustani.]] '''Kishawishi''' ni tendo la kumvuta binadamu ...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 14:45, 19 Januari 2011

Kishawishi ni tendo la kumvuta binadamu kutenda jambo. Mara nyingi maana yake ni mbaya, yaani ni kumvuta atende dhambi.

Adamu na Eva wakishawishiwa katika bustani.

Kishawishi kinaweza kujianzia au kutokana na watu wengine, lakini dini, kama vile Ukristo, zinaweza kuona nyuma yake hasa uwepo wa nguvu za giza, hususan shetani au ibilisi.

Adamu na Eva

Katika Biblia kishawishi cha kwanza kiliwapata na kuwashinda Adamu na mke wake Eva. Tukio hilo maarufu kwa jina la dhambi ya asili limeathiri binadamu wote.

Yesu

Injili zinasimulia pia vishawishi vilivyompata Yesu, hasa vitatu vilivyosababishwa na shetani jangwani, ambavyo Yesu alivishinda moja kwa moja na hivyo kutuelekeza namna ya kuvishinda vilevile.

Baba Yetu

Sala ya Baba Yetu ambayo Yesi aliwafundisha mitume wake inamalizika kwa kuomba ushindi dhidi ya vishavishi na ya Yule Mwovu (Math 6:13).