Agnes wa Asizi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Agnes wa Asizi''' (1197 au 1198 - 16 Novemba 1253) alikuwa mdogo wa kwanza wa Klara wa Asizi. Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama [[m...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 12:05, 28 Februari 2011

Agnes wa Asizi (1197 au 1198 - 16 Novemba 1253) alikuwa mdogo wa kwanza wa Klara wa Asizi.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira.

Maisha

Alikuwa binti wa pili kati ya watatu wa Favarone wa Offreduccio Scifi; mama yake Ortolana alikuwa wa ukoo wa kisharifu wa Fiumi na binamu yake Rufino ni mmmojawapo kati ya wenzi watatu wa Fransisko.

Alimfuata dada yake Klara wiki mbili tu baada ya huyo kukimbia nyumbani (18 Machi 1212) ili atawe nyuma ya Fransisko wa Asizi, mwanzilishi wa Ndugu Wadogo. Pamoja, walishinda upinzani mkali wa baba yao na ndugu wengine.

Ndipo Fransisko alipowahamishia kwenye kikanisa cha San Damiano karibu na Assisi ambacho alikuwa amekarabati kwa mikono yake.

Baada ya wanawake wengine kujiunga, monasteri yao ikawa asili ya Utawa wa Mt. Klara.

Mwaka 1219 Agnes aliteuliwa na Fransisko kama abesi wa monasteri ya Monticelli, karibu na Firenze, ambayo ikazaa monasteri nyingine Italia kaskazini, kama vile Mantova, Venezia na Padova.

Mwaka 1253 Agnes alirudishwa San Damiano wakati wa kihoro cha dada yake, akamtumikia hadi mwisho.

Mwaka huohuo, mwenyewe alifariki, tarehe 16 Novemba.

Kwa wakati huo mama yao Ortolana, na mdogo wao Beatrice, walikuwa wameshafariki katika monasteri hiyohiyo.

Heshima baada ya kifo

Masalia ya Agnes yanatunzwa katika Kanisa la Mt. Klara mjini Assisi, yalipohamishiwa pamoja na yale ya Waklara wote wa kwanza.

Papa Benedikto XIV aliruhusu Wafransisko kuadhimisha sikukuu yake kila tarehe 16 Novemba.