Michoro ya Kondoa : Tofauti kati ya masahihisho
Content deleted Content added
nyongeza |
No edit summary |
||
Mstari 1:
[[Picha:Kondoa.jpg|thumb|Mchoro mwambani.]]
'''Michoro ya Kondoa''' ni kundi la michoro kwenye kuta za mapango katika [[wilaya]] ya [[Kondoa]], [[mkoa]] wa [[Dodoma]] nchini [[Tanzania]].
Mapango au nusumapango haya zaidi ya 150 yanapatikana mfululizo kwenye vilima vinavyotazama mtelemko wa [[Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki]]. Mfululizo huo una urefu wa kilometa 9 na uko kama kilometa 20 kaskazini kwa Kondoa.
Michoro hii inaonyesha picha za watu, wanyama na uwindaji. Hii inatazamwa kutoa ushuhuda wa namna ya maisha ya wachoraji waliokuwa wawindaji hasa.
Hakuna mapatano kama michoro hii ilikuwa sehemu ya [[ibada]] za kuomba mafanikio katika [[uwindaji]] au labda ilikuwa namna ya kusimulia habari za maisha haya au labda tu [[sanaa]] ya awali bila ya makusudi.
Aina nyingine za michoro zinaonyesha tu [[milia]], [[duara]] au alama za kimsingi.
Wataalamu wengine huamini ya kwamba picha hizi zilichorwa tangu miaka 1500 iliyopita na jamii za wawindaji waliokalia eneo hili, lakini wengine husema inaewezekana ni za zamani zaidi, labda hata miaka 10,000.
Michoro inafanana na michoro kwenye [[mwamba]] inayopatikana katika [[Afrika ya Kusini]] na katika milima ya [[Sahara]].
Kuna dalili ya kwamba sehemu ilichorwa na mababu wa [[Wasandawe]] na [[Wahadzabe]] wa leo, ambao walihifadhi [[desturi]] ya kuchora mwambani hadi miaka ya karibuni na walikuwa wawindaji hadi juzijuzi.
Mwaka [[2006]] eneo hilo liliingizwa katika orodha ya [[Urithi wa dunia]].
Mahali pazuri pa kuangalia michoro kadhaa kwa urahisi ni [[kijiji]] cha [[Kolo]] kilichopo kwenye [[barabara kuu]] kati ya [[Babati (mji)|Babati]] na [[Kondoa (mji)|Kondoa]]. Kutoka hapo si mbali hadi sehemu kadhaa penye michoro. Wageni wakatakiwa kujiandikisha kwenye kituo cha hifadhi ya mambo ya kale katika kijiji.
==Viungo vya nje==
|