Majadiliano:Ukristo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 20:
Yohana alitabiriwa katika Malachi 4:4 kwambwa atakuja Eliya nabii kabla ya haijaja siku ya Bwana... Na wafuasi wa Yesu walimuuliza Yesu kuhusu huyo Eliya ni Yohana mbatizaji, aliyekamatwa na kufungwa na Herode kwa matakwa ya binti Herodi? Naye Yesu akazia kwamba ndivyo katika Yohana 11:14. Sasa inawezekanaje kwamba yule Eliya nabii kuwa ni Yohana. Hiki ni kati ya vielelezo adimu vilivyomo kwenye Biblia vyenye kuonyesha kwamba Roho ya mtu huweza kutwaa mwili tena na kuzaliwa kupitia tumbo la mwanamke. Inasadikika injili za mwanzo zilikuwa na mifano mingi ambapo Yesu mwenyewe alizungumza hivyo wazi wazi kwa wanafunzi wake. Ndio maana kuna wakati walimuuliza kama mtu kuzaliwa na mapungufu kimaumbile ni matokeo ya dhambi alizotenda kabla kuzaliwa mahala pengine(?). Hivyo Yohana aliishi na kuenenda na roho ya Eliya yule yule alipata kuwepo siku za Nyuma. Hii ni dalili ya kwamba roho hupitia mzunguko wenye kubeba tohara na mafunzo na kutakasika kufikia kioo madhubuti cha Utukufu wa Uliondani, yaani utukufu wa mbingu. Upande wa majia wa maisha ya hapa duniani ni wenye kuweza kuleta majia na hata kubadili hali mbaya za masumbuko na kukata tamaa kuwa utukufu wa juu usio na kasoro. Hivyo siri ya Kristo ni kuleta mbingu mpya na nchi mpya kupitia kiungo cha kristo. Ndio maana Neno; katika utangullizi wa Yohana una sura mbili Yesu kama binadamu na Yesu aliye Kristo yaani aliyezaliwa mara ya pili kwa roho. Na yeye Yohana mwandishi anakili alimwona Yesu kama neno halisi atokaye kwa Mungu na tena aliyejaa neema na Kweli ( Yohana 1:1-14 ).
 
Ahadi ya Musa kuhusu Kristo ilikuwa ni yenye kutegemea sana Wana wa Israeli watampokeaje Masiha. Ikiwa watambua; basi agano lake lingelitimilizwa na mambo ya kale yangelilikoma. (Paulo anazungumza kuhusu torati na Kristo katika Wagalatia 3:6-29)Na kama hawatamtambua basi wataamshambulia kama msaliti wa mifumo ya Musa yaani Torati. Lakini wale watakaompokea wanakuwa ndio walengwa halisi... Nao watalikuwa ndio wateule wenye kurithi nchi ya kweli ya ahadi, ufalme wa kweli(Yohana 1:11). Wengi walimkataa masiha, na hiyo ikawa ndo laana na mikosi kwa waisraeli hadi hii leo. Waisraeli walivamiwa na kupelekwa uhamishoni nje ya nchi yao ambayo kwa karne nyingi imeshikiliwa na wageni na wavamizi. Miaka mingi imepita lakini bado hakuna amani yerusalemu.
 
'''MAFUNDISHO YA YESU:'''
Mstari 81:
 
:Pia nitahitaji ufundi wa kuweka marejeo kwa kila neno lenye kuhitaji!
 
----
Kazi inaendelea !
 
Ninajitahidi kuipata makala sura thabiti hata kwa mtu yeyote ambaye anataka kuchunguza mapokeo na falsafa ya ndani ya Ukristo... Kuna vingi siwezi kusema moja kwa moja lakini kwa ufundi wa kutumia masimulizi ya kihistoria, ninatumaini itawezekana kubainisha, kwa jinsi yake. Maana mie pia ni mchunguzi tu, nasi muumini.
 
mpaka kwenye kanisa la kati, nimekuwa nikirejea kwenye biblia yenyewe zaidi... Naona sasa naingia kwenye historia sasa :( ... Nakaribisha yeyote ambaye anaweza kusaidia maneno machache, tusaidiane kuhariri pia :)
 
Kanisa Leo ninatazamia iwe na sura mulikaji juu ya hali ya sasa kutokana na mchetuzi wa Asili ya Ukristo, si tu kwa nje; aghalabu na dhamira zake pia zimulikwe na ndio sababu kwanini niliona ulazima wa kuchimba Ukristo kwa ndani pia.
 
Tofauti ya msingi wa makala za habari na zile za dini ama falsafa; ni katika kugusa kiini cha chimbuko ki roho... Mtu akikwepa tu hiko kiini. Basi mashauri yote yanabakia kuwa kama 'red herrings', jambo ambalo linaleta mianya ya tetesi na masimulizi kihistoria yasiyo ulazima (Kama si chakula cha mawazo tu) na hata uzushi usio na maana ya kimsingi na migongano wa kiitikadi na dhana.
 
Basi tuwe makini na historia za kweli kabisa na tunachokielewa juu ya hicho...
 
Ahsante !--[[User:Moses|Moses]] 07:54, 24 Juni 2007 (UTC)
Return to "Ukristo" page.