Infidel dogs and infidel bitches do not deserve articles nor p.b.u.h. after their names MY CROSSWIKI JIHAD: http://toolserver.org/~luxo/contributions/contributions.php?user=Aminullah&blocks=true&lang=en
[[Picha:Black Hole Milkyway.jpg|thumb|300px|Uchoraji wa shimo nyeusi jinsi wataalamu wanaiwaza. Hadi leo hakuna picha halisi ya shimo nyeusi.]]
'''Shimo jeusi''' ([[Kiingereza]]: ''black hole'') ni jina kwa eneo kwenye [[anga ya ulimwengu]] lenye [[graviti]] kubwa kiasi kwamba hata [[nuru]] haiwezi kutoka nje yake. [[Nadharia ya uhusianifu]] inatabiri ya kwamba gimba lenye masi kubwa iliyokandamizwa katika eneo dogo litasababisha "shimo jeusi". Eneo hili lazungukwa na upeo usioonekana lakini mipaka ya upeo huu ni kama mstari ambao kila kitu kinachoupita hakiwezi kurudi tena kwa sababu kinavutwa mno na graviti ya shimo jeusi. Eneo hili laitwa "jeusi" kwa sababu nuru yote inayofika upeo huu inamezwa kabisa hakuna inayorudishwa tena.
Kwa hiyo hadi sasa haikuwezekana kutazama shimo jeusi moja kwa moja. Lakini wataalamu wa [[fizikia]] waliwahi kuyatabiri mashimo haya.
Katika miaka ya nyuma [[falaki]] imeangalia mahali pengi ambako mwendo wa [[nyota]] za eneo fulani si kawaida unaelezwa kwa kuwepo kwa shimo jeusi katika sehemu hizi maana yake graviti yake inaathiri mwendo wa nyota au mawingu ya gesi ya angani na kuzivutia kwake. Mwendo huu wa magimba katika mazingira ya mashimo meusi unaonekana kwa wanafalaki.
Inaaminiwa ya kwamba shimo jeusi linatokea wakati wa kufa kwa [[nyota]] kubwa lenye masi inayozidi masi ya [[jua]] letu mara tatu au zaidi.