Kanisa la Moravian Tanzania : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Infidel dogs and infidel bitches do not deserve articles nor p.b.u.h. after their names MY CROSSWIKI JIHAD: http://toolserver.org/~luxo/contributions/contributions.php?user=Aminullah&blocks=true&lang=en
d Masahihisho aliyefanya Aminullah (Majadiliano) yalirejeshwa hadi sahihisho la mwisho na Kipala
Mstari 1:
[[Image:USVA headstone emb-27.jpg|thumb|200px|Mwanakondoo mwenye bendera ya ushindi ni ishara ya Kristo mfufuka na sehemu ya nembo la KMT]]
'''Kanisa la Moravian Tanzania''' ('''KMT''') ni muungano wa majimbo ya [[Kanisa la Moravian]] nchini [[Tanzania]]. Makao makuu yapo [[Mbeya]] mjini. Idadi ya Wakristo ilikadiriwa kuwa 410,000 mnamo mwaka 1998.
 
==Majimbo ya KMT==
 
Kuna majimbo manne ya KMT ambayo ni
* [[Kanisa la Moravian Kusini Tanzania|Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini]] (Moravian Church in Southern Tanzania) - makao makuu ni [[Rungwe]]
* [[Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Magharibi]] (Moravian Church in Western Tanzania) - makao makuu ni [[Tabora]]
* [[Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi]] (Moravian Church in South-Western Tanzania) - makao makuu ni [[Mbeya]]
* [[Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Rukwa]] (Moravian Church in Tanzania Rukwa Province) - makao makuu ni [[Sumbawanga]]
 
Kila jimbo ni kanisa kamili la kujitegemea.
 
Pamoja na hayo kuna majimbo matatu ya misioni (misheni) ambayo hayakufikia hali ya kujitegemea kikamilifu bado yakishirikiana kila moja na jimbo mzazi. Haya ni Jimbo la Misioni Mashariki ya Tanzania na Zanzibar (mzazi: Jimbo la Magharibi - Rungwe), Kanisa la Moravian Ziwa Tanganyika – Jimbo la Misheni (Mzazi: Jimbo la Magharibi - Tabora) na Jimbo la Misheni Kaskazini (Mzazi: Jimbo la Kusini-Magharibi - Mbeya).
Kwa pamoja KMT inaendesha [[Chuo Kikuu Teofilo Kisanji]] na kutoa Kiongozi Kalenda ya Moravian. Kazi nyingine ya pamoja ni kutolewa kwa "[[Kiongozi Kalenda]]" ambayo ni chaguo ya maneno ya [[Biblia]] kwa kila siku.
 
==Historia==
 
Kazi ya [[Wamoravian]] ilianza Tanzania mnamo mwaka 1891 [[wamisionari]] wa kwanza kutoka [[Ujerumani]] walipofika [[Rungwe]] katika eneo la [[Wanyakyusa]]. Kutoka Unyakyusa kazi ilipanuka kwa kuunda vituo huko [[Utengule]] (Mbeya)]] (kwa [[Wasafwa]]) na [[Mbozi]] (kwa [[Wanyiha]]).
 
Kazi katika magharibi ya nchi ilianza 1897 Wamoravian walipokabidhiwa kituo cha [[Urambo]] kilichowahi kuanzishwa na [[shirika la misioni la London]] (LMS).
 
Ndiyo chanzo cha majimbo ya Kusini (Rungwe) na Magharibi (Tabora).
 
Jimbo la Kusini Magharibi lilitengwa na lile la Kusini mwaka 1976.
 
Jimbo la Rukwa lilijitegemea na lile la Tabora mnamo 1986.
 
Hasa katika mkoa wa Mbeya kanisa la Moravian ni kubwa kati ya madhehebu ya [[Waprotestanti|Kiprotestanti]].
 
==Viungo vya Nje==
 
*[http://www.moravian.or.tz/ Tovuti ya KMT pamoja na majimbo ya Morabian Tanzania]
*[http://www.moravian.or.tz/moravian.htm Ukurasa wa KMT]
*[http://www.moravian.or.tz/Address.pdf Orodha ya watendaji na vitengo vya KMT]
 
 
[[Category:Dini katika Tanzania]]]]
[[Category:Moravian]]