Kanisa la Moravian : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Infidel dogs and infidel bitches do not deserve articles nor p.b.u.h. after their names MY CROSSWIKI JIHAD: http://toolserver.org/~luxo/contributions/contributions.php?user=Aminullah&blocks=true&lang=en
d Masahihisho aliyefanya Aminullah (Majadiliano) yalirejeshwa hadi sahihisho la mwisho na Riccardo Riccioni
Mstari 1:
{{unganisha|Wamoravian}}
 
[[File:AgnusDeiWindow.jpg|thumb|300px|<center><br />[[Nembo]] la Kanisa la Moravian (Unitas Fratrum) linamwonyesha [[Mwanakondoo wa Mungu]]. ''(Dirisha lenye kioo cha rangi katika kanisa la Moravian huko Winston-Salem, NC)''</center>]]
'''Kanisa la Moravian''' (pia: '''Umoja wa Ndugu''' kutoka jina la kihistoria la [[Kilatini]] "'''''Unitas Fratrum'''''") ni [[madhehebu]] ya [[Uprotestanti]] yaliyoanzishwa mwaka [[1722]] katika [[Ujerumani]] na [[wakimbizi]] kutoka [[Moravia]].
 
Baadaye yakaenea katika nchi nyingi kwa juhudi kubwa za [[umisionari|kimisionari]]; leo hii idadi kubwa ya [[Ukristo|Wakristo]] Wamoravian huishi katika [[Tanzania]].
 
Katika mafundisho yake hukazia [[ekumeni|umoja wa Wakristo]] na ushirikiano kati ya madhehebu mbalimbali, [[imani]] ya Mkristo binafsi, uenezaji wa imani ya kikristo na [[muziki]].
 
Nembo lake ni alama ya [[Agnus Dei|mwanakondoo wa Mungu]] anayeshika [[bendera]] ya ushindi pamoja na maandishi ya [[Kilatini]] ''Vicit agnus noster, eum sequamur'' inayotafsiriwa kama "[[Mwanakondoo]] wetu ameshinda, tumfuate" (kwa Kiingereza "Our Lamb has conquered, let us follow Him").
 
==Muundo==
Kanisa hilo linajitawala kwa utaratibu wa ki[[sinodi]] kwenye ngazi ya kila jimbo (linalolingana na [[dayosisi]] katika makanisa mengine).
 
Majimbo ya Moravian hushirikiana kwenye ngazi ya [[taifa]] kama kuna majimbo zaidi ya moja katika nchi; kwa mfano majimbo ya [[Tanzania]] hushirikiana katika "[[Kanisa la Moravian Tanzania]]".
 
Majimbo yote ya dunia hukutana kila baada ya miaka 7 kwenye "Sinodi ya Umoja" na kuchagua "Kamati ya Umoja" (Unity Board).
 
Moravian wana ngazi 3 za utumishi wa kiroho ambao ni [[shemasi|dikoni]], [[kasisi|presbiteri]] na [[askofu]].
 
Askofu ana mamlaka ya kiroho tu, hana mamlaka ya kiutawala isipokuwa kama anachaguliwa kwa muda kuwa mjumbe wa kamati ya uongozi katika jimbo lake. Vinginevyo utawala hufuata utaratibu wa kisinodi maana watumishi viongozi wanachaguliwa na sinodi kwa muda wakitekeleza taratibu zilizoamuliwa na sinodi au kamati zake.
 
==Historia==
Wamoravian wenyewe huona chanzo cha kanisa lao tarehe [[1 Machi]] [[1457]]. Siku hiyo kundi la wafuasi wa [[Yohane Hus]] waliungana katika [[kijiji]] cha [[Kunvald]] ([[Bohemia]]) kuwa umoja wa ndugu wa Kikristo, wakajiita kwa Kilatini "Unitas Fratrum" (yaani "Umoja wa Ndugu").
 
Kundi hili la Kunwald walikuwa kitengo kimoja cha harakati iliyoanzishwa na Hus miaka 50 iliyopita. Hus alitaka kutengeneza makasoro katika [[Kanisa Katoliki]] lililokuwa kanisa pekee halali katika sehemu kubwa ya [[Ulaya]] wakati ule. Aliitwa kwenye [[Mtaguso wa Konstanz]] akahukumiwa na kuchomwa moto mwaka [[1415]].
 
Wafuasi wake katika Bohemia na [[Moravia]] ([[Ucheki]]) walichukua [[silaha]] wakaanza kujihami na kipindi cha [[vita vya kidini]] vya wenyewe kwa wenyewe kilifuata.
 
Waliokutana Kunwald walikuwa wafuasi wa mafundisho ya Hus waliochoka na mauaji na vita wakiona kutumia silaha hakulingani na mafundisho ya [[Yesu Kristo]]. Walitaka kuishi pamoja kwa kuiga mfano wa maisha ya Wakristo wa kwanza.
 
Huu Umoja wa Ndugu ulienea haraka Bohemia na Moravia. Wali[[tafsiri]] [[Biblia]] katika [[lugha]] yao, wakatunga kitabu cha pamoja cha nyimbo za kiroho kwa matumizi katika [[ibada]] za kanisa na pia [[katekisimu]].
 
Kutoka kanisa la kale walipokea vyeo vya dikoni, presbiteri na askofu. Askofu wao wa kwanza alibarikiwa na askofu wa [[Kanisa la Wavaldo]].
 
Baada ya kustawi vizuri kanisa hili la Umoja wa Ndugu au "Ndugu wa Bohemia na Moravia" lilipata matatizo makali wakati wa [[Vita ya miaka 30]] na baadaye.
 
Baada ya vita hivyo ni madhehebu 3 tu yaliyokubaliwa katika [[Ulaya ya Kati]]: Wakatoliki, [[Walutheri]] na [[Wareformed]]. Umoja wa Ndugu ulipigwa marufuku, sehemu kubwa ya maeneo walipoishi waumini wake iliwekwa chini ya watawala Wakatoliki waliofunga makanisa yao na kuwalazimisha watu wote kuhudhuria [[misa]] katoliki pekee.
 
Katika hali hiyo Umoja wa Ndugu uliendelea kwa siri lakini polepole wengi walikimbilia nchi jirani walipovumiliwa kwa kiwango fulani.
 
Moravian si kanisa pekee linaloona vyanzo vyake katika ule Umoja wa Ndugu wa Bohemia, lakini ni kanisa pekee lenye uhusiano wa moja kwa moja kihistoria na kanisa hilo la zamani.
 
Kati ya wakimbizi hao kilikuwepo kikundi kutoka jimbo la Moravia lililohamia [[Ujerumani]] sehemu za [[Saksonia]]. Hapa walipokelewa na mtawala mdogo aliyeitwa [[Nikolaus Ludwig von Zinzendorf]]. Huyo alikuwa mmoja kati ya makabaila wadogo katika Ujerumani ambao walisimamia eneo dogo sana lakini walikuwa na [[uhuru]] wa kujiamulia kwa sababu walikuwa moja kwa moja chini ya [[Kaisari]] wa [[Dola Takatifu la Kiroma]] jinsi milki ya Ujerumani ilivyoitwa kwa muda mrefu.
 
Zinzerdorf alizaliwa katika [[familia]] ya Walutheri na tangu utoto aliguswa na imani ya [[uamsho]] wa Kilutheri unaoitwa [[upietisti]]. Lakini alijua watu wa kila aina, aliwasiliana pia na maaskofu Wakatoliki kadhaa akiheshimu namna yao ya imani katika Kristo.
 
Alipokuwa na umri wa miaka 22 Zinzendorf alinunua eneo la mashamba penye kijiji 1 lilikuwa utemi wake mdogo. Hapa aliwapokea wakimbizi kutoka Moravia akawapa ardhi ya kujengea kijiji chao cha "[[Herrnhut]]". Zinzendorf aliwaruhusu kuendeleza urithi wao akashirikiana nao. Wakimbizi wengine waliopaswa kuondoka kwao kwa sababu za [[dini]] walifika pia.
 
Mnamo [[Agosti]] [[1727]] wakazi wa Herrnhut walifanya mapatano kati yao kuhusu maisha ya Kikristo. Huu ulikuwa mwanzo wa "Umoja wa Ndugu ulioanzishwa upya". Zinzendorf hakutaka kuanzisha kanisa jipya; alilenga zaidi [[umoja]] wa kiroho unaokubali Wakristo wa madhehebu mbalimbali. Hivyo Herrnhut kulikuwa na vitengo vitatu ndani ya umoja: Wamoravia, Walutheri na Wareformed.
 
Kati ya misingi ya umoja ulikuwa utaratibu wa kutovuta waumini kutoka makanisa mengine kujiunga nao hata kama wahubiri wa Herrnhut walizunguka kote kwa nia ya kuamsha imani hai katika Kristo kati ya wafuasi wa makanisa au madhehebu yote ya kikristo. Kwa hiyo Kanisa la Moravian katika sehemu zake asilia (yaani Ulaya ya Kati) linajua shirika zake za Moravian pamoja na shirika za marafiki wanaoendelea kuwa Wakristo wa kanisa la kilutheri au kireformed.
 
Kwa sababu hiyo umoja mpya ulikua polepole. Makabaila waliopenda mwelekeo huo waliwakaribisha kuanzisha vijiji katika maeneo yao na kwa njia hii vijiji vya ndugu vilianzishwa katika sehemu mbalimbali za Ujerumani na pia [[Poland]]. Kwa jumla walijulikana kama "watu wa Herrnhut" hata wakijiita wenyewe "ndugu" tu au "Umoja wa Ndugu".
 
Katika utawala wake Umoja wa Ndugu uliendelea kutumia muundo wa Umoja wa kale: dikoni, presbiteri na askofu kama vyeo vya watumishi. Uongozi ulikuwa mikononi mwa wazee.
 
Mwaka [[1742]] sinodi ya umoja ilimchagua Yesu Kristo mwenyewe kuwa "mzee mkuu" wa kanisa hili.
 
Katika miaka ya kwanza walikuwa na ushirikiano wa namna ya kwamba [[wanaume]] na [[wanawake]] waliishi peke yao kadiri ya [[jinsia]]; hata [[mume]] na [[mke]] hawakuishi pamoja. Watoto walilelewa kwa pamoja baada ya kufikia umri wa miaka 2.
 
Lakini baada ya miaka makumi kadhaa waliacha muundo huu waliendelea tu kwa muda zaidi na maisha ya pamoja kwa [[vijana]] ambao hawakuoa au kuolewa bado.
 
Walikaza sana [[kazi za mikono]] na kuwafundisha vijana [[ufundi]] wakasifiwa na kutafutwa kwa ubora wa kazi yao lakini mwanzoni mapato yote yalikuwa kwa ajili ya mfuko wa umoja.
 
==Misioni na Uenezaji wa Kimataifa==
Mwaka [[1732]] mkabaila [[Denmark|Mdenmark]] rafiki wa Zinzendorf alitembelea Herrnhut akiongozana na mtumishi wake Anton mwenye asili ya [[Afrika]]. Anton aliwahi kuwa [[mtumwa]] katika [[visiwa vya Karibi]] aliyepelekwa Denmark na kuwa mtumishi huru wa mkabaila. Anton aliwasimulia habari za hali ya kusikitisha ya watumwa walionyimwa [[haki za kibinadamu]], uhuru na hata haki ya kusali kanisani. Hapo ndugu 2 walijitolea kwenda Karibi hata wakipaswa kuwa watumwa ili kuwahudumia watu hao. Walifika 1732 kwenye kisiwa cha [[St. Thomas]] wakaanza kuhubiri kati ya watumwa wenye asili ya Afrika.
 
Hii ilikuwa chanzo cha kazi ya [[misioni]] ya kanisa la Moravian ambalo ni kanisa la kwanza la Kiprotestanti lililokubali wajibu wa kueneza [[Injili]] kati ya watu wasiojua imani ya Kikristo bado.
 
Eneo la pili walipoitwa kuhubiri ilikuwa [[Greenland]] kati ya [[Waeskimo]]. Ndugu wengine walikwenda [[Marekani]] walipowalenga wenyeji asilia yaani [[Wahindi Wekundu]]. Maeneo mengine walipofika katika [[karne ya 18]] ni pamoja na [[Surinam]], [[Afrika Kusini]] na katika majimbo ya Milki ya [[Urusi]] kando ya [[Bahari Baltiki]] yaani [[Latvia]] na [[Estonia]].
 
Mwisho wa [[karne ya 19]] walialikwa pia kuanza kazi katika [[koloni]] changa la [[Afrika ya Mashariki ya Kijerumani]] (yaani sehemu kubwa ya [[Tanzania]] ya leo pamoja na [[Rwanda]] na [[Burundi]]) walipofika mwaka [[1891]]. Waliowaalika walikuwa viongozi wa misioni ya Kilutheri ambao waliona nafasi kubwa ya kuhubiri wakikosa watu waliokuwa tayari kwenda Afrika kwa hiyo walikumbuka sifa za misioni ya Herrnhut wakapiga hodi huko.
 
==Kanisa la Moravian duniani==
Mwanzo wa [[karne ya 21]] idadi ya Wakristo Wamoravian duniani ni takriban 900,000. Wengi wanaishi Afrika na idadi kubwa iko Tanzania penye majimbo 4 kamili na majimbo 3 ya misioni.
 
Herrnhut siku hizi ni ushirika katika [[Jimbo la Moravian Ulaya Bara]] linalojumlisha Ujerumani, [[Uholanzi]], [[Uswisi]] na [[Skandinavia]]. Hata huko idadi kubwa ya Wakristo ni Wamoravian waliohamia Uholanzi kutoka Surinam (iliyokuwa koloni la Uholanzi) au watoto wao na wengi wao wana asili ya Afrika.
 
===Majimbo===
Kiutawala kanisa hili linajua ngazi za Jimbo la Umoja (Unity Province), Jimbo la Misioni (Mission Province) na Maeneo ya Misioni (Mission Area). Tofauti zinatokana na kiwango cha kujitegemea kwa kila sehemu. Kila Jimbo la Umoja linajitegemea kabisa; Jimbo la Misioni bado linasimamiwa na jimbo lingine katika shughuli kadhaa na Eneo la Misioni liko kabisa chini ya jimbo fulani.
 
====Majimbo ya Umoja====
*Alaska
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Marekani Kaskazini|Marekani Kaskazini]]: [[Greenland]], [[Kanada]] na majimbo ya kaskazini za [[Marekani]]
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Marekani Kusini|Marekani Kusini]]: Majimbo ya Kusini ya Marekani
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Britania|Uingereza]]: [[Uingereza]] na [[Eire Kaskazini]]
* [[Kanisa la Moravian Jimbo la Kongo|Kongo]]
* [[Kanisa la Moravian Jimbo la Zambia|Zambia]]
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Costa Rica|Costa Rica]]
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Ucheki|Ucheki]]
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Karibi Mashariki|Karibi]]: [[Trinidad]], [[Tobago]], [[Barbados]], [[Antigua]], [[St. Kitts]], na [[Virgin Islands]]
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Ulaya Bara|Ulaya Bara]]: Estonia, Ujerumani, Uholanzi, Denmark, Uswidi, Uswisi
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Honduras|Honduras]]
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Jamaika|Jamaika]]
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Nikaragua|Nikaragua]]
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Afrika Kusini|Afrika Kusini]]
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Suriname|Surinam]]
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Rukwa]]
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Tanzania]]
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi Tanzania]]
*[[Kanisa la Moravian Jimbo la Magharibi Tanzania]]
 
====Majimbo ya Misioni====
* [[Guyana]]
* Tanzania - [[Ziwa Tanganyika]]
* [[Labrador]]
* [[Zambia]]
* [[Malawi]]
* Tanzania Mashariki & [[Zanzibar]]
* Tanzania Kaskazini
 
====Maeneo ya Misioni====
*Burundi, *[[Belize]], *[[Cuba]], *[[Guyana ya kifaransa]] *[[Kenya]], *[[Peru]], *Rwanda, *[[Uganda]]
*'''Asia Kusini''' ([[India]], [[Ladakh]], [[Nepal]], [[Assam]]) - inasimamiwa na Jimbo la Britania kwa niaba ya Umoja.
===Mradi wa Umoja===
*'''Star Mountain Rehabilitation Centre''', [[Ramallah]], [[Palestina]] ni kazi kwa ajili ya watoto [[walemavu]] [[Waarabu]] inayosimamiwa na jimbo la Ulaya Bara kwa niaba ya Umoja.
 
[[Jamii:Moravian]]
 
[[af:Morawiese kerk]]
[[cs:Moravští bratři]]
[[da:Herrnhutiske Brødremenighed]]
[[de:Herrnhuter Brüdergemeine]]
[[en:Moravian Church]]
[[eo:Unuiĝo de fratoj]]
[[es:Hermandad de Moravia]]
[[et:Hernhuutlus]]
[[fi:Herrnhutilaisuus]]
[[fr:Frères Moraves]]
[[ja:モラヴィア兄弟団]]
[[ko:모라비안]]
[[lv:Brāļu draudzes]]
[[mk:Моравска црква]]
[[nl:Evangelische Broedergemeente]]
[[no:Brødremenigheten]]
[[pl:Bracia morawscy]]
[[pt:Igreja Moraviana]]
[[ro:Frații Moravi]]
[[ru:Моравская церковь]]
[[sv:Herrnhutism]]
[[zh:摩拉维亚弟兄会]]