Afrika ya Mashariki ya Kiingereza : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 3:
'''Afrika ya Mashariki ya Kiingereza''' lilikuwa jina la eneo la [[Kenya]] lililowekwa chini ya [[utawala wa ulinzi]] wa [[Uingereza]] kuanzia mwaka 1895 hadi 1920 [[BK]].
 
Wakati wa mashindano ya kugawa [[Afrika]] kati ya madola ya [[Ulaya]] [[Kampuni ya Kifalme ya Kiingereza kwa Afrika ya Mashariki]] ilianza shughuli zake katika eneo hili kwa kibali cha sultani ya [[Zanzibar]] kuanzia mwaka 1888. Kampuni hiyo ilitakiwa kuwa na mamlaka juu ya eneo hili kwa kusudi la kufanya biashara lakini uwezo wake haukutosha kutimiza shughuli hasa maandalizi ya kujenga [[reli ya Uganda]] kati ya [[Mombasa]] na [[Kampala]].
 
Baada ya kuazimia kujenga reli [[Uingereza]] iliona haja ya kulinda eneo la reli hiyo ndipo ikatangaza eneo lote kati ya Mombasa na Uganda kuwa chini ya ulinzi wake kuanzia tarehe 01.07.1895. Huo ndiyo mwanzo wa koloni la Afrika ya Mashariki ya Kiingereza ambalo baadaye liliitwa Kenya. Eneo hilo baadaye lilipanuliwa zaidi hadi kukutana na maeneo yaliyokuwa chini ya utawala wa [[Italia]] ([[Somalia]]) na [[Ethiopia]] upande wa Kaskazini, utawala wa ushirikiano wa [[Misri]] na Uingereza ([[Sudan]]). Upande wa kusini mpaka ulifuata mapatano na [[Afrika ya Mashariki ya Kijerumani]].