Tofauti kati ya marekesbisho "Wapangwa"

585 bytes added ,  miaka 13 iliyopita
no edit summary
(mpangilio)
Chakula chao ni ugali wa mahindi, ulezi na mtama kidogo. Kitoweo cha vyakula hivyo ni maharage, samaki, nyama na jamii ya mboga mboga. Kinywaji chao ni pombe (ukhimbi) yaani kangala, komoni, ulanzi ambao hugemwa kutoka katika mmea uitwao mlanzi.
 
Hulima mazao mbalimbali katika maeneo ya miinuko na mabondeni kandokando ya mito. Ni wafugaji wa ng'ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe (kitimoto). Pia hulima mazao ya biashara kama kahawa, chai, pareto, mahindi.Kabila hili pia hupata matunda ya asili kama vile;masada,savula,makuhu,mahofita,minhingi,vudong'o na nisongwa.
Usafiri wao ni wa chombo kiitwacho ngwichili ambacho kinatengenezwa kwa kutumia miti asilia.Nyumba zao za asili kwa sasa ni za matofali ya udongo ya kuchoma na kuezekwa kwa bati,hata hivyo nyumba zao za asili zinajengwa kwa kutumia miti asili kugandikwa kwa udongo wa mfinyanzi na kuezekwa kwa nyasi aina ya hunji na lihanu.Mavazi yao ya asili ni nguo zilitengenezwa kwa ngozi za wanyama pamoja na magome ya miti ya misambi ambayo hupondwapondwa,hufumwa na kupakwa mono.
 
Lugha yao ni [[Kipangwa]].
Anonymous user