Paa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Paa umesogezwa hapa Paa (maana): afadhali tuwe na jina kwa makala
 
No edit summary
Mstari 1:
[[picha:Ashdod 2005, rooftop view p2.JPG|thumb|250px|Paa za mji wa [[Ashdod]] katika Israeli penye mvua kidogo]]
#REDIRECT [[Paa (maana)]]
[[Image:Zakopane-schronisko-2.jpg|thumb|Paa ya vigae vya ubao nchini [[Poland]]]]
'''Paa''' ni eneo la juu la [[nyumba]] ambalo linatumika kuziba eneo la ndani lisionekane kutoka juu na pia kuzuia jua na [[mvua]], [[theluji]] na [[jua]] visiingie ndani.
 
Kuna aina nyingi za paa na hizi zinategemea mazingira ya nyumba hasa [[hali ya hewa]] na pia teknolojia inayopatikana.
 
==Paa kufuatana na mazingira==
Katika mazingira penye mvua nyingi kidesturi paa inahitaji mtelemko ili maji yasikae na kuingia ndani. Kama mazingira yana upepo mkali si vizuri kuwa na mtelemko mno maana watu waliweka mawe juu ya paa kwa kusudi la kuimarisha paa dhidi ya upepo mkubwa.
 
Lakini katika mazingira kavu pasipo na mvua nyingi watu hupendelea paa ambayo ni tambarare. Paa tambarare inaruhusu kuitumia kama eneo la nje. Hasa katika nchi za joto watu hupenda kulala juu ya paa wakati wa usiku kama joto ni kubwa mno ndani ya nyumba. Ni pia mahali ambako vyakula kama matunda vinaweza kukaushwa katika jua ilhali yako mbali na wanyama au wezi wanaotembea chini. Hata hivyo kwa kawaida taa tambarare huwa na mtelemko kidogo ili maji ya mvua kama inatokea inatelemka kirahisi zaidi.
 
Teknolojia ya kisasa inaruhusu kuwa na taa tambarare hata katika mazingira penye mvua nyingi. Hapa paa hujengwa kwa [[saruji]] iliyoimarishwa kwa [[feleji]] pamoja na kemikali zinazozuia maji na kuziba paa kabisa. Faida yake ni ya kwamba ghorofa ya juu moja kwa moja chini ya paa ya nje ina nafasi kubwa inaweza kutumiwa.
 
==Sehemu za paa==
Paa huwa na sehemu mbili ambazo ni maunzi yake ya ndani halafu ganda la nje.
 
Maunzi ya ndani ya paa kwa kawaida hulala juu ya kuta za nyumba. Yanatengenezwa kwa kutumia bao, na tangu karne ya 19 pia kwa kutumia vyuma au feleji.
 
Kuna njia nyingi za kupata ganda la nje. Katika sehemu nyingi za dunia watu walitumia manyasi yanayofungwa pamoja. Kama hayatengenzwi vizuri sana kwa kutumia manyasi za pekee paa ya aina hii inavuja kirahisi inahitaji matengenezo ya mara kwa mara. Lakini penye manyasi yenye umbo la mrija kama [[gugumua]] kuna paa imara sana; zinaendelea kutumiwa hata katika nchi za kaskazini kama Denmark, Ujerumani au Uingereza.
 
Lakini kwa jumla watu wanpendelea kuwa na ganda la nje ya paa isiyoweza kuvuja. [[Mabati]] ni njia rahisi ya kufunika paa tena nyepesi; kazi ya kufunika inaenda haraka na ganda hili si nzito kwa hiyo gharama za maunzi ya ndani si kubwa. Paa ya mabati ina hasara ya kwamba mabati yanashika kutu na kuharibika baada ya miaka kadhaa; pia hakuna kinga dhidi ya joto au baridi.
 
Vigae ni njia bora ya kufunika paa; vigae ni kama matofali vinatengenzwa kwa kutumia udongo wa ufinyanzi unaopikwa katika tanuri. Kama vimetengenezwa vizuri vinaweza kudumu karibu [[dekadi]] nyingi karibu [[karne]]. Pia vina kinga dhidi ya baridi na joto kushinda bati.
 
Kutegemeana na mazingira kuna pia mbinu tofauti; mlimani penye mawe ya kufaa kuna uwezekano kutumia pia bapa za mawe. hii inahitaji lakini ubao nyingi kwa ajili ya maunzi ya chini kwa sababu bapa za jiwe ni nzito sana.
 
 
<center><gallery caption="Outer layer" perrow="6">
Image:Njem house in Cameroon.jpg|Nyumba ya [[Kamerun]] - paa ya majani ya ndizi
Image:Niigata NCM Peasant Rice Farmers House.jpg|[[Japan]], paa ya majani ya [[mpunga]]
Image:The Elms Jersey.jpg|[[Uingereza]], bapa za jiwe.
Image:Miskolc omassa peasant house.jpg|[[Hungaria]], vigae
Image:Minenverwalter Kolmannskuppe.jpg|[[Namibia]], mabati
image:Reetdachschema.jpg|[[Denmark]], majani ya guguma
</gallery></center>
 
 
[[Category:Ujenzi]]
 
[[bn:ছাদ]]
[[be:Дах]]
[[be-x-old:Дах]]
[[bg:Покрив]]
[[ca:Coberta (arquitectura)]]
[[cs:Střecha]]
[[da:Tag]]
[[de:Dach]]
[[en:Roof]]
[[es:Cubierta (construcción)]]
[[eo:Tegmento]]
[[fr:Toit]]
[[gl:Cuberta]]
[[ko:지붕]]
[[hsb:Třěcha]]
[[hr:Krov]]
[[io:Tekto]]
[[id:Atap]]
[[is:Þak]]
[[it:Copertura]]
[[he:גג]]
[[la:Tectum]]
[[lt:Stogas]]
[[nl:Dakconstructie]]
[[ja:屋根]]
[[no:Tak (arkitektur)]]
[[nn:Tak]]
[[nrm:Teit]]
[[pnb:چھت]]
[[pl:Dach]]
[[pt:Telhado]]
[[ro:Acoperiș]]
[[qu:Wasi qata]]
[[ru:Крыша]]
[[sco:Ruif]]
[[scn:Tettu]]
[[sr:Кров]]
[[sh:Krov]]
[[su:Hateup]]
[[fi:Katto]]
[[sv:Yttertak]]
[[tl:Bubong]]
[[ta:கூரை]]
[[th:หลังคา]]
[[tr:Çatı]]
[[uk:Дах]]
[[zh:屋顶]]