Nuhu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
jamii
No edit summary
Mstari 1:
Mtu huyo'''Nuhu''' anajulikana na kuheshimiwa katika [[dini]] ya [[IsraeliUyahudi]], [[Ukristo]] na [[Uislamu]] kama mfano wa mwadilifu aliyeokolewa na [[Mungu]] katika [[safina]] wakati wa [[gharika kuu]]. Kadiri ya [[Biblia]] aliishi [[Mesopotamia]].
 
Jina lake, (kwa [[Kiebrania]] '''נח''' ''Noah'', kwa [[Kiarabu]] '''نوح''' ''Nuhu'') linatafsiriwa na [[Kitabu cha Mwanzo]] ''Mfariji'', lakini maana ya hakika zaidi ni ''Anayeendeleza'' ubinadamu baada ya gharika.
 
Mwa 6:5-9:17 inatufundisha kwamba Mungu anachukizwa na dhambi, hivyo anataka kuondoa maovu duniani ili nchi impendeze kama alivyokusudia alipoiumba. Kwa ajili hiyo zamani za Nuhu alileta maji yafunike dunia na kuzamisha waovu. Lakini alisalimisha waadilifu katika safina kubwa ya kutosha, halafu akafunga nao [[agano]] thabiti ([[Eb]] 11:7).
 
Hasa maji yanayokusudiwa kutakasa dunia yote ni yale ya [[ubatizo]] ([[1Pet]] 3:17-22), na safina ambayo iokoe watu ni [[Kanisa]], ambalo kadiri ya [[Agano Jipya]] ni la lazima kwa [[wokovu]] kama vile ubatizo unaotuingiza ndani yake.
 
Uso wa nchi ulipokwishatakaswa na maji njiwa akarukaruka akachuma tawi la [[mzeituni]] unaozaa matunda ya kutengenezea mafuta.
 
Njiwa akaonekana tena juu ya maji siku ya ubatizo wa [[Yesu]] ambapo alipakwa [[Roho Mtakatifu]] na kuyatia maji nguvu ya kutakasa watu ([[Mk]] 1:9-11; [[Tito]] 3:3-7). Maji na mafuta ndiyo mwanzo mpya kwa [[binadamu]].
 
Mara alipotoka safinani Nuhu alimtolea Mungu [[sadaka]] iliyompendeza hata akaahidi hataangamiza tena binadamu kila anapostahili.
 
Sadaka hiyo ni mfano wa ile ya Yesu msalabani, inayoadhimishwa katika [[ekaristi]], ikituondolea adhabu nyingi na kutuletea huruma ya Mungu, yaani nafasi na neema ya kutubu (Tito 2:11-14). Hatimaye kutakuwa na [[hukumu]] itakayobagua waadilifu na waovu kama siku za Nuhu ([[Math]] 24:37-41) .
 
[[Category:Watu wa Biblia]]
[[Category:Watu wa Kurani]]
[[Jamii:Manabii katika Uislamu]]
 
[[ar:نوح]]