Galaksi : Tofauti kati ya masahihisho

113 bytes added ,  miaka 11 iliyopita
no edit summary
d (r2.7.1) (roboti Ondoa: hi:आकाशगंगा)
No edit summary
'''Galaksi''' ni kundi la [[nyota]] nyingi zinazoshikamana pamoja angani zikishikwa na [[mvutano]] wao. Nyota hupatikana angani katika makundi kama mawingu makubwa sana. Kuna galaksi nyingi sana ulimwenguni. Kwa wastani kila galaksi imekadiriwa kuwa na nyota kama bilioni 100 lakini kuna galaksi kubwa na ndogo.
 
Galaksi yetu ikiwemo [[mfumo wa jua]] letu imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Sehemu ya nyota hizi zinaonekana kama kanda la kung'aa kwenye anga la usiku linalojulikana kama [[njia nyeupe]]. Umbo lake unafanana na kisahani ikiwa kipenyo chake ni [[mwaka wa nuru|miaka ya nuru]] 100,000 ikiwa na unene wa miaka ya nuru 3,000. Galaksi ya jirani iliyo karibu angani inaitwa [[Andromeda]] ina umbali wa miaka ya nuru milioni 2.5 .
 
Idadi kamili ya galaksi zote angani haijulikani. Kuna makadirio ya kwamba idadi ya galaksi bilioni inaweza kuangaliwa kwa vyombo vinavyopatikana. Hadi sasa sehemu ndogo tu imehesabiwa lakini mara kwa mara galaksi mpya zinatambuliwa kwa njia ya darubini au vyombo vya angani.