Bruno Mkartusi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|right|300px|Bruno mwanzilishi wa Wakartusi. Bruno Mkartusi (Cologne, Ujerumani, 1030 hivi - [[Serra San Bruno]...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 04:07, 8 Mei 2011

Bruno Mkartusi (Cologne, Ujerumani, 1030 hivi - Serra San Bruno, Italia, 6 Oktoba 1101) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mmonaki aliyeanzisha shirika la kitawa kwa wakaapweke ambalo linadumu mpaka leo.

Bruno mwanzilishi wa Wakartusi.

Maisha

Bado kijana alikwenda Reims (Ufaransa), ambapo mwaka 1057 askofu Gervas alimkabidhi uongozi wa shule iliyomlea. Mwaka 1076 aliacha shughuli zake shuleni na ofisini akamkimbilia mtawala mdogo Ebal wa Roucy, kutokana na askofu Manase wa Gournay kumchukia kwa sababu ya kumlaumu kwa kosa la usimoni. Aliweza kurudi Ufaransa mwaka 1080 tu, baada ya Manase kuondolewa na mtaguso maalumu.

Viungo vya nje