Tofauti kati ya marekesbisho "Bruno Mkartusi"

272 bytes added ,  miaka 9 iliyopita
no edit summary
 
Bruno Mkartusi ([[Cologne]], [[Ujerumani]], [[1030]] hivi - [[Serra San Bruno]], [[Italia]],
[[6 Oktoba]] [[1101]]) alikuwa [[padri]] wa [[Kanisa Katoliki]] na [[mmonaki]] aliyeanzisha [[shirika la kitawa]] kwa [[wakaapweke]] ambalo linadumu mpaka leo ([[Wakartusi]]).
 
Anaheshimiwa kama [[mtakatifu]]. [[Sikukuu]] yake inaadhimishwa katika tarehe ya kifo chake.
 
Bado kijana alikwenda [[Reims]] ([[Ufaransa]]), ambapo mwaka [[1057]] [[askofu]] Gervas alimkabidhi uongozi wa [[shule]] iliyomlea.
Mwaka [[1076]] aliacha shughuli zake shuleni na ofisini[[dayosisi|jimboni]] (kama [[katibu mkuu]]) akamkimbilia mtawala mdogo [[Ebal wa Roucy]], kutokana na askofu [[Manase wa Gournay]] kumchukia kwa sababu ya kumlaumu kwa kosa la [[usimoni]]. Aliweza kurudi Ufaransa mwaka [[1080]] tu, baada ya Manase kuondolewa na [[mtaguso]] maalumu.
 
=== Wito wa kimonaki ===
Katika miaka hiyo migumu, ndipo [[wito]] wake wa kimonaki ulipojitokeza. Katika barua yake mojawapo Bruno alisimulia jinsi alivyoweka [[nadhiri]] ya kujitoa [[wakfu]] kwa [[Mungu]] pamoja na marafiki wawili.
 
Kisha kurudi Ufaransa, alikwenda kwenye [[makao ya upwekeni]] ya Molesme, chini ya uongozi wa [[Roberto wa Molesme]], [[mwanzilishi]] wa [[urekebisho]] wa [[Citeaux]] wa [[Wabenedikto|shirika la mtakatifu Benedikto]]. Halafu, pamoja na wenzi sita (mapadri 4 na ma[[bruda]] 2), alitafuta mahali pa faragha kabisa ili kuanzisha [[mpnasterimonasteri]], akapewa na askofu wa [[Grenoble]], [[Ugo wa Grenoble]], ambaye alisukumwa na [[njozi]]. Eneo hilo la kufaa lilikuwa bonde katika milima iliyoitwa «Cartusia» (kwa [[Kifaransa]] «Chartreuse»).
 
=== Kartusi ===
Monasteri ilianza kujengwa katikati ya mwaka [[1084]], kwenye mita 1175 juu ya [[usawa wa bahari]]. [[Kanisa]] tu lilijengwa kwa mawe, ili liweze kuwekwa [[wakfu]], kama ilivyofanyika mwaka [[1085]].
 
Miaka sita baadaye [[Papa UrbanoUrban II]], aliyekuwa mwanafunzi wake huko Reims, alimuita [[Roma]], atumikie [[Ukulu mtakatifu]]. Bruno hakuweza kukataa, hivyo aliacha upweke kwa wenzake.
 
=== Huko Italia ===
[[Category:Waliozaliwa 1030]]
[[Category:Waliofariki 1101]]
[[Jamii:Mapadri]]
[[Category:Wamonaki]]
[[Category:Watawa waanzilishi]]
[[Jamii:Wakartusi]]
[[Jamii:Watakatifu wa Ujerumani]]
[[Jamii:Watakatifu wa Italia]]
 
[[be:Бруна Кёльнскі]]