Wagermanik : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: en:Germanic peoples
kiungo
Mstari 25:
Wagermanik walikuwa na uhamisho mbalimbali tangu karne nyingi. Majaribo ya makabila ya Kigermanik kuingia katika Italia yalirudishwa na jeshi la Roma katika karne ya 2 KK. Katika karne ya 2 BK kabila la Wagothi lilianza kuhamia kusini kutoka bonde la Vistula kuelekea [[Bahari Nyeusi]]. Hapa waligongana na Wagermanik wengine na kuwasababisha kuingia katika eneo la Kiroma kwenye [[Balkani]]. Miendo hii bado ilihusika vikundi visiyokuwa vikubwasana na Dola la Roma liliweza kuwapokea watu wa makabila haya na kuwatumia kama wanajeshi au kama walowezi waliokubali ubwana wa Kiroma ndani ya mipaka ya dola.
 
Lakini katika karne ya 4 makundi makubwa ya watu walielekea Ulaya kutoka Asia ya Kati na hao walikuwa makabila ya [[Wahunni]]. Walienea kwa nguvu wakasababisha [[uhamisho mkuu wa Ulaya]] kati ya Wagermanik walioendelea kuhamia upanda wa kusini na magharibi. Kuanzia karne ya 4 hadi manmo mwaka 700 makabila mengi ya Wagermanik walianza kuhamahama katika Ulaya ama kwa sababu walishambuliwa na Wahunni au Wagermanik wengine au kwa sababu waliona nafasi ya kuingia katika maeneo tajiri zaidi ya majirani waliodhoofishwa na vita kutokana na harakati hii ya uhamisho mkuu.
 
Dola la Roma lilishindwa kujitetea dhidi ya watu wengi hao waliofika kwenye mipaka yake likaanza kuwaruhusu kuingia ndani ya eneo lake na kuwapa ardhi ya kulima na kujenga makazi. Kadri jinsi uwezo wa Roma ulipungua makabila ya Wagermanik waliowahi kuingia walianza kuasi dhidi ya mamlka ya Kiroma na kuhama tena. Katika miaka 150 ya kwanza ya uhamisho mkuu uwezo wa Dola la Roma uliporomoka kabisa na mwaka 476 wanajeshi wa Kigermanik katika jeshi la Kiroma walimpindua Kaisari na kuchukua utawala katika Italia.