Tofauti kati ya marekesbisho "Karl Marx"

29 bytes added ,  miaka 9 iliyopita
d
roboti Nyongeza: am:ካርል ማርክስ; cosmetic changes
d (roboti Nyongeza: am:ካርል ማርክስ; cosmetic changes)
Tangu [[1842]] alikuwa mwandishi mkuu wa [[gazeti]] la ''Rheinische Zeitung'' mjini [[Köln]]. Alisimama upande wa wafuasi wa [[demokrasia]] dhidi ya utawala wa watemi na wafalme katika Ujerumani.
 
Kutokana na upinzani huo [[serikali]] ya [[Prussia]] ilimkataza asiandike tena kwenye magazeti, hivyo alihamia [[Ufaransa]]. Alipokaa mjini [[Paris]] alianza kuandika juu ya [[ujamaa]] kama ukamilisho wa demokrasia.
 
Baada ya kuhamia [[Brussels]] katika [[Ubelgiji]] alitunga pamoja na Engels kijitabu cha [[Manifesto ya Chama cha Kikomunisti]] (Ilani ya kikomunisti) alimotangaza [[imani]] yake ya kwamba "historia ya jamii zote ni historia ya mapambano ya matabaka". Alichora picha ya historia ambako jamii ya kikabaila imezaa ngazi mpya ya [[ubepari]]; hapo alitabiri kwamba ubepari utazaa tena mbegu wa uharibifu wake na utafuatwa na ujamaa au ukomunisti. Ukomunisti utakuwa na jamii bila matabaka na bila [[utawala]]. Aliona ya kwamba wafanyakazi kama [[tabaka]] linalozalisha [[utajiri]] wanapaswa kuchukua utawala mikononi mwao kwa njia ya [[mapinduzi]] akawaalika, "Wafanyakazi wa nchi zote muungane!".
 
[[af:Karl Marx]]
[[am:ካርል ማርክስ]]
[[an:Karl Marx]]
[[ar:كارل ماركس]]
44,008

edits