Unajimu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 16:
Watu wa kale walikuwa hodari sana kutazama nyota na kutambua mabadiliko yao katika mwendo wa wakati. Hali hii haieleweki kirahisi na watu wa leo waliozoea nuru ya taa za umeme wakitumia wakati wa usiku kutazama TV au kompyuta. Lakini kwa watu wa kale -jinsi ilivyo hadi leo kwa watu wengi vijijini au porini- nyota na mwezi zilikuwa taa hasa wakati wa usiku.
 
Uhusiano ulioonekana kati ya mabadiliko ya nyota na mabadiliko ya majira yalianzisha elimu ya [[kalenda]] pamoja na elimu ya [[unajimu]] na falaki[[astronomia]].
 
Kwa wazee hawa ilionekana kama nyota fulani inatawala majira, hali ya hewa na hivyo maisha ya kibinadamu kwa sababu maisha ya jamii yalitegemea majira na mwendo wa mvua, ukame, baridi au joto. Hapo ni asili ya kuziangalia nyota kama miungu au pepo zenye uwezo fulani. Hasa tabia ya hali ya hewa ya kuchelewa au kuwahi kidogo ilijenga imani ya kwamba kuchelewa kwa mvua ni dalili ya hasira ya mungu yule anayeonekana kama nyota fulani.