Tofauti kati ya marekesbisho "Hadithi za Mtume Muhammad"

18 bytes added ,  miaka 8 iliyopita
d
roboti Badiliko: id:Al Hadits; cosmetic changes
d (r2.7.1) (roboti Nyongeza: el:Χαντίθ)
d (roboti Badiliko: id:Al Hadits; cosmetic changes)
'''Hadithi''' au Sunnah ni maneno na vitendo ambavyo Mtume Muhammad alikuwa akisema au akifanya katika kipindi hiki cha [[Utume]]. Hadithi hizi ni moja ya miongozo ya kiimani kwa Waislamu. Hadithi hizi zinajumuisha pia mambo aliyoyaona au kuyasikia katika muda wa Utume wake akalinyamazia kimya au akawa hakulipinga na akalikubali.
 
[[Muhammad]] aliishi miaka kama arobaini bila kuwa na Imani ya [[Mungu]]. Kisha Mwenyezi Mungu akamletea mjumbe kutoka kwake aitwaye [[Jibrili]] inayeaminika kuwa ndiye aliyempa aya zilizoko katika msahafu wa [[Waislamu]], [[Kurani]]. Inaelezwa kuwa Jibrili alimpa Muhammad aya hizo kwa muda wa miaka ishirini na tatu mpaka alipofariki dunia akiwa na umri wa miaka 63.
 
Hadithi za Mtume Muhammad zimekusanywa katika vitabu vingi sana na [[wanazuoni]] mbali mbali wa Hadithi, lakini vitabu vya hadithi ambavyo ni muhimu na vinategemewa na wengi katika [[Uislamu]] ni hivi vifuatavyo:
 
== Vitabu vya Hadithi ==
* ''1- Sahih Al-Bukhari''
* ''2- Sahih Muslim''
* ''3- Sunan An-Nasai''
* ''4- Sunan At-Tirmidhi''
* ''5- Sunan Ibn Majah''
* ''6- Sunan Abu Daud''
* ''7- Muwatt'a Ibn Maalik''
* ''8- Musnad Ahmad bin Hanbal''
 
 
Kuna Hadithi aina nne kulingana na fahamu na kutegemewa kwa msimulizi wa hiyo Hadithi. Hadithi Sahihi, Hadithi Hasan (Nzuri), Hadithi Dhaifu, na Hadithi Maudhu'u (Hadithi ya Uwongo). Vile vile, kuna aina nyingine za Hadithi zilizogawanyika kwa mujibu wa mambo mengine kama kwa mujibu wa wapokezi, au mfululizo wa wasimulizi, au idadi ya wasimulizi katika kila sehemu ya mfululizo, au kwa mujibu wa simulizi yenyewe na msimulizi wake..
 
== Hadithi kwa mujibu wa fahamu na kutegemewa kwa msimulizi ==
* Hadithi Sahihi huwa imesimuliwa kutegemewa ukweli wake na dini yake na ambaye anafahamu nini anasimulia, na kuieleza hadithi kama alivyoipokea kutoka kwa Mtume Muhammad.
* Hadithi Hasan au Nzuri huwa inajulikana asli yake na wasimulizi ni watu maarufu.
* Hadithi Dhaifu huwa ile isiyofikia daraja ya Hasan, kwa sababu ya upungufu wa mmoja katika wasimulizi, au mfululizo wa wasimulizi haufikii mpaka kwa Mtume unakatika kwa mojawapo ya Masahaba, au mmoja katika wasimulizi kuwa si wa kutegemewa, na kuwa kuna kasoro fulani katika mambo haya.
* Hadithi Maudhu'u (ya Uwongo) ni ile hadithi iliyobuniwa ikatiwa katika Hadithi za Mtume, na huwa kawaida inakwenda kinyume na Qurani au Hadithi nyenginezo Sahihi au Hasan, au kutonasibiana na maneno yake Mtume au kuwa msimulizi wa Hadithi hii ni mwongo, au kuwa msimulizi hakukutana na yule ambaye amesema amepokea kwake katika mfululizo wa wasimulizi waliotajwa, au kuweko kasoro fulani katika maelezo au matukio yaliyotajwa ndani ya Hadithi hio.
 
== Hadithi kwa mujibu wa wasimulizi ==
* Hadithi Qudsi ni ile hadithi ambayo Mtume Muhammad ameisimulia kutoka kwa Mola wake
* Hadithi Marfu'u ni hadithi iliyopokewa na mfululizo wa wasimulizi na kufikishwa mpaka kwa Mtume
* Hadithi Mauquf ni ile hadithi iliyosimuliwa na masahaba lakini wasiseme kuwa wameipokea kutoka kwa Mtume mwenyewe.
* Hadithi Maqtu'u ni ile hadithi iliyokatika silsila au mfululizo wake
 
* http://www.hadiths.eu
 
[[CategoryJamii:Uislamu]]
 
[[Category:Uislamu]]
 
{{Link FA|id}}
[[he:חדית']]
[[hu:Hadísz]]
[[id:Al Hadits]]
[[is:Hadíða]]
[[it:Hadíth]]
43,953

edits