Mboo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Badiliko: mzn:دول
No edit summary
Mstari 1:
[[Picha:Human_penis_both_flaccid_and_erect.jpg|thumb|Mboo wa [[binadamu]] kabla na baada ya kusisimka.]]
 
'''Mboo''' (pia: '''Uume''') ni kiungo cha [[uzazi]] cha kiume ambacho hupitisha [[shahawa]] yenye [[mbegu]] kutoka ma[[pumbu]] kupitia [[kifuko cha akiba]] kwa kuingizwa katika [[kuma]].

Mboo pia hutumika kupitisha [[mkojo]].
 
Muundo wa uume ni [[misuli]] aina ya [[sifongo]] yenye [[neva]] nyingi. Kukiwa na [[msisimko]] [[damu]] inajaa nafasi zilizomo na kusababisha uume utanuke na kusimama imara na wima.
 
==Mabadiliko ya ubalehe==
Ingawa kila mtu ni [[mwanamume]] au [[mwanamke]] tangu atungwe (kadiri alivyo na [[kromosomu Y]] au la), kabla ya [[kubalehe]] tofauti hazionekani sana, isipokuwa katika [[viungo vya uzazi]]. Kumbe muda unafika wa watoto kuanza kukomaa kijinsia: ndipo tofauti zinapojitokeza wazi.
Kutoka [[utoto]]ni kuingia [[utu uzima]] kuna mabadiliko ya haraka katika [[viungo]], [[hisia]] na [[roho]]. Kama ilivyo kwa [[viumbe hai]] wote, [[ustawi]] huo unaweza ukawahi au kuchelewa, lakini kwa kawaida unatokea kati ya [[umri]] wa miaka 12 na 16. [[Wasichana]] wanawahi kuliko [[wavulana]], na [[Wazungu]] kuliko [[Waafrika]], lakini mabadiliko ni yaleyale, nayo yanafanyika hatua kwa hatua.
 
Katika hayo, mengine yanamfurahisha [[kijana]], lakini mengine hayampendezi, anayonea [[aibu]] hata kuyafadhaikia hasa asipoyaelewa. Bila ya shaka anahitaji msaada wa [[walezi]] aweze kukabili hayo yote bila ya kuvurugika kiasi cha kupotoka.
 
Kwanza [[mvulana]] anajikuta akirefuka haraka na kupata [[misuli]] mikubwa; [[kifua]] kinapanuka. Papo hapo [[sauti]] yake inaanza kupasuka na kuwa nzito, [[ndevu]] zinaweza zikaota, na vilevile [[malaika [[sehemu za siri]], [[kwapa]]ni na pengine kifuani. Hali ya [[ngozi]] inakuwa ikikwaruzakwaruza hasa [[uso]]ni, na [[chunusi]] hujitokeza.
 
Katika hatua ya mbele mabadiliko yanahusu zaidi viungo vya uzazi vinavyokua na kuanza kazi ambayo kwa kawaida itaendelea moja kwa moja, kumbe kwa [[msichana itakoma kati ya miaka 40 na 50.
 
Mabadiliko ya mwili yanaendana na mengine ya nafsi yanayofanya [[tabia]] iwe tofauti na ile ya awali. Hisia zinabadilika kadiri mwili unavyozidi kutengeneza [[chachu]] ([[homoni]]) zinazomfanya kijana aelekee namna ya [[baba]] au mama zake.
 
Mvulana anajikuta akivutiwa na uzuri wa wasichana, na kupenda kuwajua zaidi, kuongea nao n.k. Anapenda kuwagombeza na kuwaonea ili aonyeshe uwezo na [[nguvu]] alivyonavyo. Katika hatua hiyo anakuwa [[mvivu]] na mzito katika kutembea na mara nyingi hajali [[unadhifu]]. Kumbe msichana anazidi kupenda [[sifa]] na kujiremba.
 
[[Akili]] pia inapevuka na kumfanya kijana apende kuwa na maoni maalumu kuhusu mambo mbalimbali, hata kubishana na wengine. Pia apende mabadiliko, [[ujuzi]] mpya n.k. Ndiyo sababu kijana si mwepesi kupokea ma[[shauri]] na maoni ya wakubwa, asije akajisikia tena [[mtoto]] huku akipenda kutambulika amekuwa [[mtu mzima]]. Kwa ajili hiyo anatamani kufanya yale wanayoyafanya wakubwa (kuvuta [[sigara]], kurudi nyumbani [[usiku]] n.k.), kushirikiana na [[rika]] lake na hata kujiunga na makundi ya wanaomzidi katika shughuli zao ([[genge]], [[timu]] n.k.) ingawa pengine hazifai ([[uhuni]], [[bangi]] n.k.).
 
Hatimaye kuna mabadiliko upande wa roho: kati ya mawazo mengine, kijana anajitafutia msimamo mpya kuhusu maswali makuu ya maisha: anataka kuwa na [[falsafa]] na [[dini]] yake. Shida ni kwamba [[usahihi]] wa majibu unategemea sana [[uadilifu]] wa maisha: kijana akifuata [[anasa]], akili inapofuka na [[imani]] inapotea.
== Mabadiliko ya viungo vya uzazi ==
[[Uume]] ([[mboo]]) wa [[mvulana]] unakua, lakini kwa kiasi tofauti kati ya mtu na mtu. Ni muhimu kila mmoja ajipokee alivyo hata katika kiungo hicho, bila ya kuhangaika wala kuona [[aibu]] kwa sababu, eti ni kidogo.
 
Kusimika kwa uume si jambo jipya kwa kuwa [[utotoni]] limeshatokea kawaida kutokana na [[kibofu]] kujaa [[mkojo]]. Ila sasa linaweza kutokea kwa sababu mpya, yaani [[jinsia]].
 
Kusimika kunajitokeza na kupotea haraka kutegemeana na hali iliyopo. Hali hiyo inaweza kutokea bila ya mtu kutaka, kwa mfano [[usiku]] au pia [[mchana]] kati ya watu ikimfanya aone [[haya]].
 
Upande wa [[maadili]] tusisababishe hali hiyo bila ya lengo jema, kama vile kumtibu [[mgonjwa]], kutoa [[ushauri nasaha]] au kujielimisha kuhusu [[jinsia]]. Kwa hiyo tukwepe kwa kawaida yale yote yanayoweza kusisimua, kama vile mawazo, maneno, masomo, mitazamo na vitendo mbalimbali kuhusu jinsia. Mvulana anahitaji kujifunza [[nidhamu]] ya namna hiyo.
 
Mashauri mengine ni kutovaa [[kaptura]] wala [[suruali]] zinazobana, na kuficha kwa [[adabu]] hali hiyo ikitokea, lakini bila ya kuiogopa wala kudhani ni [[dhambi]].
 
[[Mapumbu]] yanaanza kutengeneza [[mbegu za kibinadamu]] kwa wingi sana: hizo ni ndogondogo na zina umbo kama la [[viluwiluwi]] vya [[chura]], yaani vina vichwa na mikia tu.
 
Vichwa ndivyo vinavyoleta [[viini vya urithi]] wa baba. Mikia kazi yake ni kusaidia tu kusukuma mbegu ndani ya [[tumbo la uzazi]] mpaka zikutane na [[kijiyai]] cha [[mama]], halafu inapotea ndani ya kijiyai. Mbegu zikiwa tayari zinahifadhiwa kwanza katika [[kifuko cha akiba]], karibu na kibofu, zikisubiri msisimko wa kijinsia ili zitoke kwa njia ya uume na kuanza mashindano ya kutafuta kijiyai, zikisaidiwa na majimaji ambayo yanaitwa [[shahawa]] na kutengenezwa ndani ya kifuko. Shahawa inafuata [[mshipa wa mkojo]] bila ya kuchanganyikana nao.
 
Shahawa inaweza ikatoka hata nje ya tumbo la uzazi la [[mke]], lililo [[shabaha]] yake, kwa kuwa inalenga [[uzazi]] hasa. Inaweza ikatokea k.mf. kutokana na [[ndoto]] za usiku, bila ya mtu kukusudia; huyo anaweza akazinduka mara au kutambua [[asubuhi]] tu kilichotokea. Kwa vyovyote asihangaike kwa kuwa hilo ni jambo la kawaida lililopangwa na [[Mungu]] ili kumsaidia [[mwanamume]] asiye na mwenzi. Maana mbegu zake kadiri zinavyoongezeka katika kifuko cha akiba zinataka kutoka, hivyo zinamuelekeza kwenye matendo ya kijinsia. Basi, kwa ndoto hizo mbegu zinapungua bila ya dhambi, na [[vishawishi]] vinakosa ukali wake. Ni suala la kusubiri tu na kuwa na hakika kwamba havitadumu muda mrefu kwa nguvu ileile.
 
Mvulana anapotokwa na shahawa kwa mara ya kwanza ni dalili ya kuwa si mtoto tena, bali ana [[uwezo wa kuzaa]]: kwa hiyo awajibike kama [[mtu mzima]] kuhusu uwezo mpya aliojaliwa. Hasa azingatie kuwa uwezo wake huo bado ni mbichi: ingawa unaweza kusababisha mimba, mimba hiyo itaendelea kwa shida au kufa kabisa.
 
Ubichi ni mkubwa zaidi upande wa [[nafsi]], kwa kuwa mvulana hajawa tayari kubeba mzigo wa [[familia]] mpya. Ndiyo sababu asichezee uwezo huo, bali ajiandae kuwa [[baba]] safi siku za mbele: ajipatie [[elimu]] au [[ufundi]] fulani, akomae kiutu na kutunza afya yake ya mwili na ya nafsi.
 
Kumbe akijiingiza mapema katika masuala ya [[ngono]], anahatarisha [[heshima]] yake pamoja na afya, kwa kuambukizwa maradhi yanayoweza yakasababisha [[utasa]] au kwa kuzaa kwa shida kabla ya wakati wa kufaa.
 
{{mbegu-anatomia}}
 
[[Jamii:Viungo vya mwili]]
[[Jamii:Jinsia]]
 
[[af:Penis]]