Kampeni za Kivita katika Afrika ya Mashariki (Vita ya Kwanza ya Dunia) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
nyongeza kadhaa
No edit summary
Mstari 7:
Mikakati ya jeshi la kikoloni la Kijerumani lililoongozwa na Luteni Koloneli (baadaye ''Meja-jenerali'') [[Paul Emil von Lettow-Vorbeck]] ililenga kuwalazimisha wapinzani hasa Waingereza kutumia wanajeshi wengi iwezekanavyo katika Afrika kwa shabaha ya kuwazuia wasipatikane kwenye vita ya Ulaya.
 
Mkakati yake ilifaulu kiasi cha kwamba Waingereza walipaswa kuleta vikosi vikubwa kutoka [[Uhindi ya Kiingereza]] na [[Afrika Kusini]] kupigania kempeni ya Afrika ya Mashariki. <ref>Holmes 2001, p. 359.</ref><ref>Strachan 2003, p. 642.</ref>
 
==Awamu la kwanza: 1914-1915==
Katika awamu la kwanza la vita jeshi la Kijerumani lilishambulia [[reli ya Uganda]] na vituo vya mpakani na Kenya. Waingereza walijibu kwa kukusanya walowezi wao katika Kenya bila kufaulu kuwazuia Wajerumani walioteka mji wa [[Taveta]]. Hiyvo Waingereza walichukua askari 12,000 Wahindi na 2 Novemba 1914 walishambulia [[Tanga]]. Lakini askari Waafrika wa jeshi la Kijerumani waliwashinda Tanga na baadaye pia [[Longido]] karibu na [[mlima Kilimanjaro]], wengine huko [[Yassini]].
[[picha:Battle of tanga.jpg|thumb|250px|Mapigano ya Tanga]]
Hapo Waingereza waliamua kuchukua wanajeshi Wazungu kutoka Afrika Kusini chini ya amri wa jenerali [[Jan Smuts]] waliofika Kenya hadi mwisho wa 1915. Wakati huohuo Wabelgiji walipanga pamoja na Uingereza kupeleka vikosi vya jeshi lake Force Publique katika Kongo mpakani wa magharibi.