Kampeni za Kivita katika Afrika ya Mashariki (Vita ya Kwanza ya Dunia) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
nyongeza kidogo
Mstari 24:
Alipeleka jeshi lake katika eneo kusini ya mstari Daressalaam-Morogoro-Iringa pasipo na njia nzuri akitegemea Waingereza wasingeweza kutumia usafiri kwa malori na reli.
 
Hadi hapa maendeleo ya vikosi vya maungano yalikuwa na matatizo mengi. Walitegemea hasa askari Wazungu na Wahindi waliozoea kusafiri na mizigo mikubwa ya vyakula, nguo na hema na kwa hiyo walihitaji [[hamali|mahamali]] wengi. Hivyo maendeleo yao yalikuwa polepole wakahitaji chakula kingi kulisha askari pamoja na mahamali. Askari pamoja na mahamali walikuwa wageni ambao hawakuzoea vema hali ya hewa na magonjwa hivyo walisumbuliwa na ugonjwa. Kwa mfano kikosi cha 9th South African Infantry ilifika kwa askari Wazungu 1,135 mwezi wa Februari 1916 na hadi Oktoba ni 116 pekee waliobaki tayari kwa vita, ingawa kikosi hiki hakikuona mapigano na wote wengine walikufa au bila uwezo kutokana na magonjwa.<ref>Falls, Cyril. The Great War. New York: Capricorn Books. 1961, p. 253</ref>

Kinyume chake Lettow Vorbeck aliwategemea hasa askari Waafrika waliokuwa na mahitaji madogo waliojua nchi na kuzoea magonjwa ya mazingira. Waingereza walitumia askari Waafrika hasa kwa kulinda reli ya Uganda kwa sababu mwanzoni walikosa imani katika uwezo wao.
 
==Awamu la tatu: vita ya porini==