Angahewa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
jamii
d r2.7.2) (roboti Badiliko: br:Atmosferenn; cosmetic changes
Mstari 1:
[[Picha:Angahewa_tabaka.png|thumb|300px|right|Tabaka za angahewa ya dunia]]
'''Angahewa''' ni ganda la [[gesi]] za [[hewa]] zinazozingira dunia yetu zikishikwa na [[nguvu mvutano]] yake. Angahewa inakinga uhai duniani kwa kupunguza [[mnururisho]] wa [[urujianimno]] wa jua, kutunza halijota duniani kwa kuakisisha mawimbi [[infraredi]], kupunguza tofauti kati ya baridi na joto na kuwapa [[wanyama]] na [[mimea]] viwango vya [[oksijeni]] na [[nitrojeni]] wanayohitaji.
 
Magimba ya angani mengine kama [[sayari]] au [[jua]] huwa pia na aina za angahewa ingawa gesi zake ni tofauti na duniani.
 
Gesi zilizopa katika angahewa ya dunia ni hasa [[nitrojeni]] (78 %) na [[oksijeni]] (21 %) pamoja na viwango vidogo lakini muhimu vya [[arigoni]] (0.9 %), [[kaboni dioksidi]] (0.035 %), mvuke wa [[maji]] na gesi mbalimbali.
 
Angahewa haina mwisho kamili inazidi kuwa hafifu jinsi inavyofikia juu. Asilimia 75 ya masi ya hewa yake iko katika tabakatropo hadi kilomita 11 juu ya uso wa dunia.
 
== Halijoto na tabaka za angahewa ==
Sehemu za angahewa zina baridi au joto zaidi kutegemeana na kimo. Tukipaa juu ya uso wa dunia halijoto inazidi kuwa baridi, baadaye joto tena, kadiri jinsi tunavyopaa. Mabadiliko ya halijoto yanafuata muundo wa tabaka zinazootofautishwa na kiwango cha joto au baridi kinachopimwa.
 
Kwa jumla inawezekana kutofautisha tabaka 5 ambazo ni
* [[Tabakatropo]] (troposphere) - inaanza kwenye uso wa dunia na kuishia mnamo kilomita 7 (juu ya ncha za dunia) - 15 (juu ya sehemu za [[tropiki]]) juu yake; baridi inazidi jinsi unavyopaa juu (kwa hiyo ni baridi mlimani kushinda chini); mawingu yako hapa na hii ni tabaka ambako [[halihewa]] inatokea.
* [[Tabakastrato]] (stratosphere) - inaishia kwenyi kimo cha 50 [[km]]; hapa joto linaanza kuzidi tena. [[Eropleni]] kubwa zinapita hapa kwa sababu hakuna upepo mwenye nguvu inayosumbua mwendo
* [[Tabakakati]] (mesosphere) - inaishia kwa kimo cha 80 - 85 km; hapa baridi inazidi jinsi unavyopaa; kuna upepo mkali.
* [[Tabakajoto]] (thermosphere) - inaishia kwa kimo cha 500 - 600 km; joto linapanda pamoja kimo; tabaka hii ni muhimu kwa mawasiliano ya redio kwa sababu inaakisisha miale ya redio ya AM.
* [[Tabakanje]] (exosphere) - ni tabaka la nje inayoanza kati ya 500- 1000 km na kuwa hafifu kadri unayopaa juu zaidi; inafikia kilomita maelfu hadi kwa kimo cha takriban 10,000 km ambako hewa haipimiki tena
 
Tabaka za juu yaani tabakajoto na tabakanje huitwa pia [[tabakaioni]] kwa sababu [[atomi]] za gesi zake zinapatikana katika hali ya [[ioni]] zilizopoteza [[elektroni]] kutokana na kupigwa na miale ya jua iliyo bado kali sana hapo nje.
 
== Viungo vya Nje ==
* [http://www.ux1.eiu.edu/~cfjps/1400/atmos_struct.html The Atmosphere]
 
[[CategoryJamii:metorolojiaMetorolojia]]
 
[[af:Aarde se atmosfeer]]
Mstari 33:
[[bg:Атмосфера на Земята]]
[[bn:পৃথিবীর বায়ুমণ্ডল]]
[[br:Atmosfer (Douar)Atmosferenn]]
[[bs:Atmosfera]]
[[ca:Atmosfera terrestre]]