Mwerezi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'Mti wa mwerezi ni mti wenye historia katika nchi ya Lebanon. Historia ya mwerezi wa lebanon inaanzia miaka mingi nyuma kabla Yesu hajazaliwa, kwa mfano katika Z...'
 
No edit summary
Mstari 1:
Mti wa mwerezi ni mti wenye historia katika nchi ya Lebanon. Historia ya mwerezi wa lebanon inaanzia miaka mingi nyuma kabla Yesu hajazaliwa, kwa mfano katika Zaburi 92:12 "Wenye haki watastawi kama mtende,watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni". Ni mti unaostahimili hali za baridi kali na joto pia. Mwerezi hukua taratibu sana na hivyo kuufanya kuwa mti wenye mbao imara. Kwa sababu hiyo mierezi ya Lebanon imekuwa ikikatwa kwa wingi tangu enzi za mfalme Suleiman (na wafalme wengine pia)ambae aliitumia mierezi ya Lebanon katika ujenzi wa hekalu la Yerusalem. Mierezi ya Lebanon imekuwa pia ikitumiwa na wenyeji wake kutengeneza mashua ambazo ziliwawezesha kuwa wafanya biashara wa kwanza wa kimataifa. Kutokana na ukataji uliokithiri, miti ya mierezi imekuwa ni michache sana katika nyakati hizi. Kwa mfano kusini mwa Lebanon ni ngumu hata kuamini kwamba kuliwahi kuwa na misitu yenye miti mikubwa na kuiletea sifa nchi ya Lebanon. Imebaki miti michache katika maeneo ya kaskazini karibu na mpaka wa Syria. Kutokana na historia iliyotukuka ya mti wa mwerezi, mti huo umewekwa katikati ya bendera ya nchi ya Lebanon na kuwa miongoni mwa alama muhimu za taifa la LebanonLebano.