Gowee : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: ca:Corythaixoides
Nyongeza matini
Mstari 17:
''[[Gowee Uso-mweusi|Corythaixoides personatus]]''
}}
'''Gowee''' ni [[ndege]] wa [[jenasi]] ''[[Corythaixoides]]'' katika [[familia (biolojia)|familia]] [[Musophagidae]]. Jina lako linatoka sauti yao inayosikika kama “gwee” au “gowee” (Waingereza wasikia "go-away" na huitwa ndege hawa [[w:Go-away-bird|Go-away-bird]]). WanaitwaHuitwa [[shorobo]] pia kama spishi nyingine za Musophagidae.
 
Ndege hawa wana rangi ya kijivu na nyeupe na wana kishungi kirefu. Wanatokea [[Afrika]] chini ya [[Sahara]]. Hawawezi kupuruka vizuri sana lakini hukimbia juu ya matawi ya miti. Hula [[tunda|matunda]] hasa na [[jani|majani]] na [[ua|maua]] pia, na mara chache hukamata [[mdudu|wadudu]] na [[koa]]. Hujenga tago lao kwa vijiti katika mti mwenye miiba, kama spishi ya ''[[Acacia]]'' ([[mgunga]]) au ''[[Balanites]]'' ([[mjunju]]), na jike hutaga mayai 1-4 lakini 3 kwa kawaida. Vinda wakitoka kwa mayai, wanapambwa na malaika mazito na macho yao ni wazi tayari au karibu.