Udongo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: simple:Soil
No edit summary
Mstari 8:
 
Udongo hupatikana kama tabaka juu ya mwamba unaofanya [[ganda la dunia]]. Mpaka wa chini wa udongo ni pale ambako mwamba mtupu unaanza; mpaka wa juu ni uso wa ardhi. Tabaka la udongo unaweza kuwa na unene wa kilomita kadhaa au sentimita chache tu.
 
==Tabaka za udongo==
Udongo mzuri huwa ndani yake na matabaka A-B-C pamoja na tabaka ya mata ogania juu yake.
 
'''O) Mata Ogania''': katika mchoro huu 2 sentimita za juu ambazo ni majani makavu na sehemu nyingine za mimea zilizokufa au kuanguka chini; hazikuoza bado kikamilifu lakini zinaendelea kuoza. Wadudu wengi wanaishi hapa wanaoendelea kuozesha mata hii.
 
'''A) Udongo wa juu:''' Tabaka ya udongo yenye kiasi kikubwa cha mada ogania ndani yake. Ndani yake kuna minyoo na vijidudu wengi wanaoendelea kula na kubadilisha mabaki ya majani yaliyomo mle kuwa madini.
 
Katika tabaka la udongo wa juu maji ya mvua inapita haraka zaidi na kwa hiyo madini yeyushi kama chuma, alumini, chumvi mbalimbali na mengine. Kutegemeana na uwingi wa mvua na hali ya udongo chini yake kiasi cha madini hizi inaweza kuwa haba zaida.
 
'''B) Udongo wa chini:''' katika tabaka hii madini yaliyoyeyushwa katika udongo wa juu zinakusanyika. Hapo ni sababu ya kwamba kulima shamba kunaongeza rutba maana kazi ya kuchimba inapeleka madini yaliyozama chini kwenda juu.
 
'''C) Mwamba mzazi:''' hii ni tabaka ya mwamba usimegeka bado. Unaitwa mwamba "mzazi" kwa sababu vipande vidogo vya matabaka ya juu via asili hapo; kwa hiyo mwamba mzazi una tabia nyingi za kikemia sawa na udongo wa juu.
 
Mizizi mirefu ya miti inaendelea kufika hadi sehemu ya juu ya mwamba mzazi na kutafuta hapa madini yeyushi zilizozama chini zaidi. Kwa njia hiyo inachangia mmomonyoko wa sehemu hii hata kama imefunikwa na udongo.
 
== Marejeo ==