Sabato : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
sahihisho picha
No edit summary
Mstari 9:
Wayahudi wakifuata dini huanza kwa sala ya jioni kwenye [[sinagogi]] halafu kwa chakula cha pekee.
 
==Msingi wa Sabato katika Biblia==
Msingi wa utaratibu wa sabatu uko katika Biblia kitabu cha [[Kutoka (Biblia)|Kutoka]] sura ya 20:8-11 katika orodha ya [[Amri Kumi]]:<br>
:''Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya mlango yako. Maana kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.''
 
Amri hii ilichukuliwa kama amri ya kutofanya kazi na kupumzika. Tabia ya pekee katika amri hii ni sharti ya kuwapa hata wafanyakazi na watumwa nafasi hii ya kupumzika. Hivyo ami hii inatazamiwa kama sheria ya kwanza ya kutunza haki za wafanyakazi.
 
==Mapokeo ya Talmudi==
Tangu kale wataalamu Wayahudi walijadili swali je kazi ni nini chini ya masharti ya amri ya sabato. Majadiliano haya yaonekana katika maandiko ya Agano Jipya kwa mfano pale ambako Yesu aligongana na [[mafarisayo]] kuhusu swali la uponyaji siku ya Sabati (Mk. 3 na penginepo).
 
Wataalamu Wayahudi waliendelea kujadiliana hadi kuorodhesha katika [[Talmudi]] aina 39 za shughuli ambazo ni marufuku siku ya Sabato.
Kwa mfano ni marufuku kuwasha moto, kuandika, kutekeleza kazi yoyote kwa chombo, kununua au kuuza kitu, kugusa hela.
 
[[Wayahudi Waorthodoksi]] hutunza masharti hadi leo. Wataalamu wameendelea kuangalia mapokeo ya Talmudi katika mazingira ya kisasa. Shart ya kutowasha moto imeendelezwa ya kutowasha taa hata za umeme ikaendelezwa kutobonyeza swichi yoyote siku ya Sabato. Lakini inaruhusiwa kutumia mitambo inayofuata saa au programu na kuwacha taa au mashine bila mtu kugusa.
 
[[Wayahudi huria]] hawachukui amri hizi vikali vile. Kwa mfano Myahudi huria asingeandika chochote kinachohusika kazi yake lakini hana tatizo la kuandika barua isiyo ya kikazi. Atajaribu kuepukana na tendo la kununua kitu dukani lakini kama kuna haja ataifanya.
 
Wayahudi wote wafundisha ya kwamba sheria zote za Sabato zaweza kuvunjwa kama maisha ya kibinadamu iko hatarini.
 
==Wakristo na Sabato==
Katika Ukristo sabato imehamishwa kwenda siku ya [[Jumapili]] isipokuwa kati ya madhahebu madogo kama [[Wasabato]]. Chanzo chake inaonekana katika taarifa ya [[Matendo ya Mitume]] 20:7 inayoonyesha ya kwamba wakati wa [[Paulo]] Wakristo walikutana siku ya kwanza. Sababu yake ilikuwa kukumbuka ufufuo wa Yesu aliyetoka kaburini siku hii ya kwanza yaani Jumapili.
 
Agano Jipya haielezi badiliko hili. Sababu inayotajwa tangu kale (lakini baada ya kipindi cha Biblia) ni ya kwamba ufufuo wa Yesu ilikuwa uumbaji mpya na hivyo katika kipindi cha Agano Jipya ile sikukuu ya agano la kwanza haisimami tena.
 
Kwa muda mrefu Jumapili iliheshimiwa kama siku ya ibada ya kikristo lakini bila masharti ya kuacha kazi. Sharti hili lilikaziwa tu katika nchi za Ulaya tangu karne ya 18 na 19.
 
{{siku za juma}}
[[Category:Uyahudi]]
[[Category:Kalenda]]
{{stub}}