Udongo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 14:
'''O) Mata Ogania''': katika mchoro huu 2 sentimita za juu ambazo ni majani makavu na sehemu nyingine za mimea zilizokufa au kuanguka chini; hazikuoza bado kikamilifu lakini zinaendelea kuoza. Wadudu wengi wanaishi hapa wanaoendelea kuozesha mata hii.
 
'''A) Udongo wa juu:''' Tabaka ya udongo yenye kiasi kikubwa cha mada ogania ndani yake. Ndani yake kuna [[minyoo]] na vijidudu wengi wanaoendelea kula na kubadilisha mabaki ya majani yaliyomo mle kuwa madini au [[kampaundi ogania]] sahili zaidi. Kwa kazi yao wanasababisha kuwepo kwa mashimo na nafasi ndogo ndani ya udongo wa juu. Nafasi hizi zinasaidia kuingia na kutoka kwa gesi na kiowevu. Kutokana na uwingi wa viumbehai hivi vidogo udongo wa juu una uwezo wa kutunza maji ya mvua ndani ya nafasi zake. Hii yote ni muhimu kwa kustawi wa mimea inayotandiza hapa mizizi yao.
 
Kwa lugha nyingine kuwepo kwa viumbehai hivi vidogo ni muhimu kwa rutba ya udongo. Uhaba wa mata ogania unasababisha pia uhaba wa viumbehai ndani ya udongo wa juu unaokosa rutba jinsi ilivyo jangwani.
 
Katika tabaka la udongo wa juu maji ya mvua inapita haraka zaidi na kwa hiyo madini yeyushi kama chuma, alumini, chumvi mbalimbali na mengine. Kutegemeana na uwingi wa mvua na hali ya udongo chini yake kiasi cha madini hizi inaweza kuwa haba zaida.