Historia ya Wapare : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 6:
Simulizi zinasema walipoingia Tanganyika, walitamani kufanya makao yao kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro, lakini wakavurumishwa na wenzao waliokuwepo hapo kabla yao, yaani Wachagga.
Wachagga hawa hawakuwa radhi kuwaruhusu Wapare hawa kuwa na makazi eneo hili, hivyo waliwafukuza kwa kupigana kama ilivyokuwa tabia ya makabila mengi hapo zamani.
 
==ASILI YA NENO WAPARE==
Wakati wa kupambana walikuwa wakiambiana, “mpare…mpare” wakimaanisha ‘mpige…mpige!’Waasu hawa wakatimka mbio na kuparamia milima ambayo sasa inaitwa milima ya Upare. Waasu wakaanza kuitwa Wapare kwa maana ya wapige!
Hizi ni hadithi zinazosimuliwa na baadhi ya Wachagga ambao ndiyo watani pekee wa Wapare, utani uliozaliwa baada ya purukushani hizo za kuingia Tanganyika.
Hata hivyo, hakuna hata Mpare mmoja anayeafiki maelezo hayo isipokuwa wanakiri kuwa walitokea Taveta ndiyo maana hata baadhi ya maneno na lafudhi yao haiko mbali sana na watu wa Taveta.
==MFUMO WA MAISHA=
Mzee Katengu Ramadhani ni Mpare. Anasimulia kuwa Wapare ni kabila lenye ujasiri na ni watu wa kupanga kabla ya kutenda. Pia anaongeza kuwa ni wavumilivu wenye kustahimili hali ngumu ya maisha ikiwa ni pamoja na njaa au kutokuwa na pesa.
===Mbiru===
Inasemekana Wapare kwa ujasri mkubwa enzi za ukoloni waliweza kujiunga pamoja na kufanya mgomo wa kukataa kodi za kikoloni zilizokithiri. Mgomo huo uliofanikiwa ulijulikana kama ‘mbiru’.
Hata hivyo, nilivutiwa zaidi alipozungumzia mfumo wa maisha waliokuwa ambao kwangu niliuona ni wenye kuwaongezea sifa katika nchi hii.
Mzee Katengu Ramadhani alisimulia kuhusu mila na desturi ya Wapare zilizowajengea taratibu za kuwa na mifumo waliyoiita ‘Ndala’, ‘Msaragambo’ na ‘Kiwili’.
Mifumo hiyo ni;
===Ndala===
Kwa mujibu wa mzee huyo neno ‘ndala’ kwa Kipare humaanisha utaratibu wa familia au watu wanaoishi jirani mno kuwa na tabia ya kula chakula kwa pamoja, kama wengi tuonavyo waislamu waliofunga na wanapofuturu pamoja.
Utaratibu wa Wapare ulikuwa kwamba kila mama anapotayarisha chakula kwa familia yake, ilibidi akitoe achanganye na chakula kingine cha wenzake na familia zote ziketi na kula pamoja. Mfumo wa ndala kwa maana ya familia kula chakula kwa pamoja unaonekana kuwa na manufaa yafuatayo.
Kwanza unajenga mahusiano mema baina ya familia na majirani katika kushirikiana. Pili kushirikiana katika kula kunachochea ushirikiano katika mambo mengine kama shida au raha.
Lakini pia watoto wanaokuzwa katika mfumo huo wanajengwa katika maadili mazuri wasiwe walafi na wachoyo maana wanazoea kuwa na wenzao na hii ndiyo sababu kabila hili lilikuwa na sifa ya kuwa wakarimu.
Watoto walifundishwa kuwa na nidhamu ya wakati wa chakula, kwa mfano kutonawa mikono au kuanza kula kabla ya wakubwa.
===Msaragambo===
Neno msaragambo linamaanisha mfumo uliokubaliwa na jamii katika kitongoji, kijiji au kata wa kushirikiana katika kufanya kazi zenye faida kwa watu wote, maarufu kwa kazi za ujenzi wa taifa.
Kwa kazi hizi ni za ridhaa zilipaswa kwanza zikubaliwe na wengi vinginevyo haikuwa rahisi mtu mmoja kuitisha wito wa kazi fulani na watu wengine kuja kuifanya.
Kazi hizi ambazo hata serikali ya awamu ya kwanza ilizikazania sana mara baada ya Tanganyika kupata uhuru, ni pamoja na ujenzi wa mashule, kuchimba visima vya maji, kuchimba barabara na kadhalika. Upo ushahidi wa kutosha kuhusu Wapare walivyotumia mfumo huu na kupata maendeleo makubwa Wilayani mwao.
Zipo barabara za Mwanga hadi Ugweno na Usangi; Ndungu hadi Mamba na Vunta; Hedaru hadi Mwala; Makanya hadi Chome,Mpirani hadi Bombo Song’ana,Gonja Maore hadi Vuje naVudee hadi Mbaga. Hata hivyo, si barabara tu lakini zahanati, na shule nyingi zimejengwa na wapare wa wilaya za Same na Mwanga na kuinua kiwango cha maendeleo yao.
Nakumbuka watu hawa si watu wapenda misaada ya mteremko ndiyo maana pamoja na kukabiliana na hali mbaya ya uhaba wa mvua mara kwa mara wamekuwa si watu wa kupiga yowe haraka.
Kazi zilizofanywa kupitia utaratibu huu wa msaragambo ziliufanya Mkoa huu wa Kilimanjaro uongoze kwa maendeleo ya barabara nzuri, ujenzi wa shule nyingi hadi katika vitongoji.
===Kiwili===
Kiwili ni msamiati mwingine wa Kipare ambao ni mfumo wa maisha walioukubali katika kuendesha maisha ya familia na jamii zao kwa kusaidiana kazi.
Kiwiri ni utaratibu ambapo familia au majirani hualikana ili kusaidiana katika kazi za kilimo, na hata mavuno hasa pale mmoja wao anapokuwa na kazi shambani mwake na kuhitaji msaada. Siku hiyo, watu hukutana na kufanya kazi hiyo waliyoitiwa, mwenye kazi huandaa chakula ambacho watu watapata baada ya kumaliza kazi.
Utaratibu huu ulikuwa na manufaa makubwa maana ulirahisisha kazi na kujenga moyo wa kusaidiana. Kiwiri pia kiliweza kuitishwa na majirani kuwalenga wazee waliochoka au wagonjwa, ambao kwa namna moja au nyingine walionekana kushindwa kumudu kazi zao za shambani.
Kupitia kazi za kusaidiana maisha ya familia nyingi za Wapare ziliokolewa na majanga ya kufikwa na njaa.
Bilashaka utakuwa umebaini kuwa zipo mila na desturi nzuri ambazo Watanzania tulikuwa nazo, lakini wageni wakatuhadaa na kutulaghai kwamba ya kwetu yote yalikuwa si mema nasi tukaanza kuyaacha.