Historia ya Wokovu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 157:
Manung’uniko ya Waisraeli katika safari yao jangwani yakawaletea adhabu nyingine, mojawapo ile ya kugongwa na [[nyoka]] wengi wenye [[sumu]] kali. Lakini walipoomba [[msamaha]], Mungu akamuagiza Musa atengeneze [[nyoka wa shaba]] na kumuinua juu ya mti ili mtu aliyeumwa akimtazama tu apate kupona (Hes 21:4-9). Ufafanuzi wa tukio hilo ulitolewa na Yesu mwenyewe: ndiye aliyeinuliwa juu ya mti wa msalaba ili watakaomtazama kwa imani wapate kuishi (Yoh 3:14-15).
 
===Kumbukumbu la SheriaTorati(sheria)===
 
Kitabu hicho cha mwisho cha Torati kiliandikwa kama miaka 600 baada ya Musa, ingawa kina namna ya [[hotuba]] tano alizoweza kuwatolea Waisraeli kabla hajafa. Kinapitia upya matukio ya wokovu ya wakati wa Musa kikifaidika na ujumbe wa manabii, hasa [[Hosea]]. Kwa msingi huo, kitabu hiki kinasisitiza sana [[upendo]] kwa Mungu, [[uaminifu]] kwa agano la mlima Sinai pamoja na tuzo na adhabu zitakazotolewa kufuatana na matendo ya Waisraeli.
Mstari 166:
Baada ya hotuba hizo, Kumb 31:1-8 inasimulia jinsi Musa alivyomuachia Yoshua uongozi wa Waisraeli wote kwa kumwekea mikono (Hes 27:12-23). Musa alifikia mpakani mwa nchi takatifu asikubaliwe kuiingia kama adhabu ya makosa yake, ila alionyeshwa yote kutoka mlimani (Kumb 32:48-52) halafu akafariki (Kumb 34). Kazi aliyopangiwa iliishia huko, mwingine akampokea na kuendeleza ukombozi wa Kimungu. Binadamu wote ni vyombo tu vinavyotumika kwa muda fulani, halafu vinaweza kuachwa. Kumbe Mungu ndiye mtendaji mwenyewe ambaye hasinzii wala halali, bali anazidi kuwashughulikia watu wake. Kwa imani hiyo tuwe daima tayari kuwaachia wengine nafasi yetu.
 
===Vitabu vinavyofuata Kumbukumbu la Torati(Sheria)===
 
Vitabu vinavyofuata katika [[Biblia ya Kiebrania]] (Yoshua, Waamuzi, Samweli na Wafalme) vinataka kuthibitisha kwamba kweli ikawa kama hiki kinavyosema: Waisraeli walipofuata agano (wakati wa [[Yoshua]]) waliteka [[nchi ya ahadi]] na kuifurahia, lakini walipozidi kuasi (wakati wa [[Waamuzi]], [[Samweli]] na Wafalme) walikuja kunyang’anywa nchi ile yote, kwanza sehemu nzuri zaidi ([[kaskazini]]), halafu ile hafifu zaidi ([[kusini]]). Hapo Waisraeli wote wakajikuta tena utumwani katika nchi ya kigeni kama kabla ya Musa, wakikosa hata [[sanduku la agano], lililopotea wakati wa maangamizi ya [[Yerusalemu]] na [[hekalu]] lake, baada ya wao kufikia hatua ya kula watoto wao kutokana na njaa.