Imani : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d r2.7.2) (Roboti: Imeongeza ky:Ишеним
No edit summary
Mstari 1:
[[Picha:Giotto - Scrovegni - -44- - Faith.jpg|160px|thumb|leftright|Mchoro wa [[Giotto]], ''Imani'', [[Padua]]]]
{{Maadili ya Kimungu}}
[[Picha:Giotto - Scrovegni - -44- - Faith.jpg|160px|thumb|left|Mchoro wa [[Giotto]], ''Imani'', [[Padua]]]]
 
Ingawa kwa [[Kiswahili]] neno '''imani''' lina maana mbalimbali (k.mf. "huruma"), ile kuu inahusiana na kitenzi '''kuamini''', kinachofanana na '''kusadiki'''. Hapo ni kukubali [[ukweli]] wa jambo lisiloweza kuthibitishwa.
Mstari 9:
 
Kadiri ya [[Mtume Paulo]] imani ikifuatana na [[tumaini]] na [[upendo]] ni [[adili]] kuu mojawapo, msingi, mzizi na chanzo cha [[wokovu]].
 
==Roho ya imani katika [[maisha ya kiroho]]==
Kila mara [[mtu]] anafuata ama [[umbile]], asipopita fikra za kibinadamu tu, ama [[imani]], anapolenga [[mbinguni]] kwa njia ya [[utakatifu]]. Roho hizo zinazotuongoza maishani ni namna maalumu za kupima, kuona, kuhisi, kupenda, kushabikia, kutaka na kutenda. Basi, roho ya imani ni kupima yote kwa mtazamo wa juu ambao unapita maumbile na kutegemea [[mamlaka]] ya [[Mungu]] katika kujifunua, na [[ukweli]] wake katika kutushirikisha [[utukufu]]. Tunaelewa zaidi roho ya imani tukiangalia iliyo kinyume chake, yaani [[upofu wa roho]] unaozuia mtu asione mambo ya Mungu isipokuwa kidunia na kutoka nje. Hivyo [[Israeli]] haikuelewa [[uteuzi]] wake kadiri ya ukweli wa Mungu ulio wa juu kuliko [[ukabila]] au [[ubaguzi]] wowote.
 
Imani ina mitazamo mipana kuliko huo kutokana na [[usahili]] wake unaoshiriki [[hekima]] ya Mungu. Juu sana kuliko mifuatano ya mawazo, ni tendo sahili ambalo tunamsadiki Mungu anayefunua na papo hapo anajifunua. Kwa tendo hilo lipitalo maumbile tunaambatana naye pasipo [[udanganyifu]] na hivyo katika [[giza]] tunalenga kutazama mambo ya Mungu, juu kuliko [[hakika]] zote za kibinadamu. Hakika inayotokana na imani tuliyomiminiwa na Mungu, inapita hata hakika ya [[akili]] tunayoweza kujipatia kwa kuzingatia [[miujiza]] inayothibitisha [[ufunuo]] wake.
 
Imani ni [[zawadi]] ya Mungu: “Kwa maana mmeokolewa kwa [[neema]], kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni [[kipawa]] cha Mungu” ([[Ef]] 2:8). Ni kama [[hisi]] ya Kiroho inayotuwezesha kusikia [[ulinganifu]] wa ma[[fumbo]] aliyotufumbulia, yaani kusikia [[sauti]] yake kabla hatujakaribishwa kumuona uso kwa uso.
 
“Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia bali [[Roho Mtakatifu|Roho]] atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kujua tuliyokirimiwa na Mungu, nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi, [[mwanadamu]] wa [[tabia ya asili]] hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni [[upuuzi]], wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini [[mtu wa rohoni]] huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. Maana, ni nani aliyefahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo” ([[1Kor]] 2:12-16). Ili ifanye hivyo imani inasaidiwa na [[vipaji vya Roho Mtakatifu|vipaji]] vya [[kipaji cha akili|akili]] na [[kipaji cha hekima|hekima]], lakini yenyewe ndiyo inayotufanya tushike [[Neno la Mungu]] pasipo udanganyifu.
 
Ingawa mafumbo yake ni ya giza kwetu, [[adili]] la imani ni bora kuliko [[ujuzi]] mwangavu walionao [[malaika]] kwa umbile lao, kwa sababu imani tunayomiminiwa inalingana na [[uzima wa milele]], kwa kuwa ndiyo [[mbegu]] yake. Malaika wenyewe walihitaji zawadi hiyo waweze kulenga [[hali ipitayo maumbile]] waliyoitiwa.
 
Mungu anapotujalia imani, anapenya [[roho]] yetu na kusema nayo si kwa mifuatano ya maneno, bali kwa [[wazo]] la [[ghafla]]. Imani ikifika, tunaachana na mfuatano wowote wa mawazo tuliokuwanao pamoja na [[sababu]] zake: tunaviweka chini ili imani ivikalie kama [[mtawala]]. Imani ikiangaza akili kwa [[mng’ao]] wa kweli zake, mara [[utashi]] unahisi [[joto]] la [[upendo]] wa Mungu.
 
==Imani tuliyomiminiwa inatakiwa kustawi hadi kifo==
 
Imani inatakiwa kukua kila [[siku]]. “Imani inaweza ikawa kubwa ndani ya [[Ukristo|Mkristo]] mmoja kuliko ndani ya mwingine, upande wa akili kutokana na hakika na [[imara]] kubwa zaidi katika kushika ufunuo, na upande wa utashi kutokana na [[utayari]] na [[utiifu]] au [[tumaini]] kubwa zaidi” kwa kuwa “imani tunayomiminiwa inalingana na zawadi ya neema, ambayo si sawa kwa wote” ([[Thoma wa Akwino]]). [[Yesu Kristo]] aliwasema wanafunzi wake kuwa “wa imani haba” ([[Math]] 6:30); kumbe alimuambia [[mwanamke]] [[Mkananayo]], “[[Mama]], imani yako ni kubwa!” (Math 15:28).
 
Imani inaweza kukua kwa [[upana]] na kwa [[dhati]] au [[nguvu]]. Inapanuka tunapozidi kujifunza yale yote [[Kanisa]] linayoyafundisha: [[wanateolojia]] wanayajua wazi, lakini si kwamba imani yao ni ya dhati na ya nguvu kadiri ilivyoenea. Kumbe tunakuta [[watakatifu]] wasiojua mengi katika hayo, lakini wanapenya mafumbo yalivyofumbuliwa na [[Injili]] kwa usahili. [[Mitume wa Yesu]] walimuomba imani hiyo waliposema, “Tuongezee imani” ([[Lk]] 17:5). Yesu akawaambia, “Yoyote mtakayoomba katika [[sala]] mkiamini, mtapokea” (Math 21:22). Tutayapokea hasa tukijiombea kwa [[udumifu]] yaliyo ya [[lazima]] au ya kufaa sana kwa [[wokovu]]wetu, kama vile [[ustawi wa maadili]].
 
==Ubora na uwezo wa imani==
 
[[Thamani]] ya imani inapimwa na matatizo inayoyashinda katika ma[[jaribu]]: “Kwa imani [[Ibrahimu]] alipojaribiwa, akamtoa [[Isaka]] awe [[dhabihu]]… yeye aliyeambiwa: Katika Isaka [[uzao]] wako utaitwa, akihesabu ya kuwa Mungu aweza [[ufufuko|kumfufua]] hata kutoka [[kuzimu]]… Kwa imani walishinda [[milki]] za wafalme, walitenda [[haki]], walipata [[ahad]], walifunga vinywa vya [[simba]], walizima nguvu za [[moto]]… Wengine walijaribiwa kwa [[dhihaka]] na mapigo, naam, kwa [[mafungo]], na kwa kutiwa [[gereza]]ni; walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa [[upanga]]; walizungukazunguka wakivaa [[ngozi]] za [[kondoo]] na ngozi za [mbuzi]], walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya – watu ambao [[ulimwengu]] haukustahili kuwa nao” ([[Eb]] 11:17-19, 33-34, 36-38). Mambo kama hayo yanatokea hata siku hizi. “Basi na sisi pia, tupige [[mbio]] kwa [[saburi]] katika yale [[mashindano]] yaliyowekwa mbele yetu, tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya [[furaha]] iliyowekwa mbele yake aliustahimili [[msalaba]] na kuidharau [[aibu]], naye ameketi [[mkono]] wa kuume wa [[kiti]] cha enzi cha Mungu” (Eb 12:1-2).
 
“Mzingatieni [[Kristo]] aliyevumilia [[upinzani]] wa namna hiyo kutoka kwa [[wakosefu]]… Hapo katika [[tabu]] yoyote mtaona [[dawa]] katika [[msalaba wa Yesu]]. Humo mtakuta vielelezo vya maadili yote. [[Gregori Mkuu]] alisema tukiyakumbuka [[mateso ya Yesu]] hatutaona chochote kuwa kigumu au cha tabu tusiweze kukivumilia kwa subira na upendo” (Thoma wa Akwino). Imani ikistawi inatufanya kwa kawaida tuzidi kuhisi [[fumbo]] la Kristo; polepole hisi hiyo ipitayo maumbile inakuwa [[sala ya kumiminiwa]] yenye kupenya na kuonja, asili ya furaha na [[amani]]: “Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini… Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu” ([[Fil]] 4:4,7).
 
==Tuishije kwa roho ya imani?==
 
Tunapaswa kuishi hivyo kwa kupima yote kwa mwanga huo wa juu: kwanza Mungu, halafu [[nafsi]] yetu, [[jirani]] na ma[[tukio]] yote.
 
Je, kuna haja ya kusema tumzingatie Mungu kwa imani? Bila ya [[shaka]]! Kwa kuwa mara nyingi tunamzingatia kwa [[dhana]] zisizo na msingi, kwa [[miguso]] ya kibinadamu mno na kwa ma[[ono]] yetu, badala ya kupitia [[ushuhuda]] alioutoa juu yake mwenyewe. Pengine hata tunaposali tunajisikiliza tu kwa kumkopesha Mungu mawazo yetu yanayotokana na [[umimi]]. [[Kujiamini kipumbavu|Tunapojiamini kipumbavu]] tunaelekea kudhani [[huruma]] ya Mungu ni kwa ajili yetu, na [[haki]] yake kwa watu tusioelewana nao. Kumbe [[kukata tamaa|tukikata tamaa]] tunatilia shaka kimatendo upendo wa Mungu kwetu na huruma yake kuu. Kwa imani tunamuona Mungu kupitia mafumbo ya maisha na mateso ya [[Mwokozi]] na kupitia [[uhai]] wa Kanisa linalofanywa upya na [[ekaristi]] kila siku. [[Jicho]] la imani linasafika zaidi na zaidi kwa [[ufishaji]] wa [[hisi]] na maono, [[maoni]] na [[matakwa]] yetu: hapo tu unakuja kuanguka polepole ule [[utaj]] wa [[kiburi]] unaotuzuia tusione mambo ya Mungu au tuone tu vivuli vyake na tata zake.
 
Tunapaswa vilevile kujitazama kwa imani. Tukijitazama kibinadamu tu, tunaona ndani mwetu [[sifa]] za umbile ambazo mara nyingi tunazizidisha. Baadaye, majaribu yakituonyesha tulivyojidanganya [[kuvunjika moyo|tunavunjika moyo]] kwa [[urahisi]]. Kumbe kwa imani tunakuja kujua [[utajiri]] upitao maumbile ambao Bwana ametutia katika [[ubatizo]] na kutuongezea kwa ekaristi, yaani thamani ya [[neema inayotia utakatifu]], ya [[uwemo wa Utatu mtakatifu]] pamoja na ukuu wa [[wito]] wa Kikristo. Tunakuja kujua pia vizuio vya ustawi wa uzima huo, k.mf. [[usahalifu]] wa mbegu ya [[uzima wa milele]] iliyopandwa ndani mwetu, na kiburi cha kipumbavu. Kwa mtazamo huo wa juu tunakuja kujua mapema [[kilema]] kinachotutawala na [[kivutio]] maalumu cha neema tulicho nacho, ambavyo cha kwanza kikomeshwe na cha pili kistawishwe.
 
Lakini tunayesahau zaidi kumtazama kwa imani ndiye jirani. Tunamtazama kibinadamu tu, tukiathiriwa na dhana zisizo na msingi, kiburi, [[wivu]] na vilema vingine. Kwa hiyo ndani yake tunakubali yale ambayo yanatupendeza kibinadamu, yanatufaidisha au kutukuza; kumbe tunahukumu yale ambayo yanatukinaisha, yanamfanya bora kuliko sisi na kutushusha. [[Dhambi]] ngapi za kuhukumu na [[singizio|kusingizia]] zinatokana na mtazamo huo uliofunikwa na utaji wa umimi! Tukijifunza kumtazama jirani kwa imani ni [[faida]] kubwa pande zote. Hapo tunakuja kuwaona wakubwa wetu kama wawakilishi wa Mungu, na kuwatii kwa moyo pasipo kuwasema. Tunaona kuwa wasiotupendeza wamekombolewa kwa [[damu]] ya Kristo, pengine ni viungo vya mwili wake vinavyokaribia moyo wake kuliko sisi: mara nyingi tunaishi miaka pamoja na watu safi tusitambue [[uzuri]] wa roho zao. Vilevile, tukija kuwatazama kwa imani wanaotupendeza, pengine tunavumbua wana [[maadili ya Kimungu]] kiasi cha kuzidisha na kutakasa [[mapendo]] tunayowaonea; pia kwa wema tunaona vizuio walivyonavyo kwa [[utawala wa Mungu]] na tunaweza kushauriana nao tusonge mbele katika njia yake.
 
Hatimaye tunapaswa kutazama kwa imani matukio yote ya maisha yetu, ya furaha na ya [[uchungu]] vilevile. Mara nyingi tunaridhika kuyaona upande wa hisi tu, au kwa akili iliyoathiriwa na dhambi. Mara chache tunayazingatia Kimungu, kwa kuona kwamba “katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema” ([[Rom]] 8:28): hata katika upinzani, matatizo makubwa yasiyotarajika na dhambi (tukiweza kujinyenyekesha kutokana nazo). Katika kukosewa haki na watu tunaweza kutambua [[haki ya Mungu]] ikiadhibu makosa ya siri ambayo hatulaumiwi na mtu; au tunahisi [[majaribu]] ya Kimungu, na [[utakaso]] unaokusudiwa kupatikana kwa njia ya hayo.
 
Kabla ya imani yetu kutakaswa kwa majaribu kadhaa ya aina hiyo, tujitahidi kukua katika imani, badala ya kupima yote kibinadamu tu. Ni lazima tujinyime mianga midogo na ya bandia ili tujaliwe ile ya juu; tuache kufuata mno akili yetu ili tuone [[uangavu]] mkuu wa mafumbo ya imani na kuishi kulingana nayo. Hivyo tunaelewa kwa nini hatutakiwi kuitikia vishawishi dhidi ya imani, bali kuvikataa au kuviruka kwa kukiri imani kwa dhati zaidi; [[Bwana]] anaviruhusu kwa maendeleo yetu tu.
 
[[Jamii:Dini]]
Line 14 ⟶ 53:
[[Jamii:Ukristo]]
[[Jamii:Maadili]]
[[Jamii:Maisha ya kiroho]]
 
[[ar:إيمان]]