Daudi (Biblia) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 8:
Kati ya matendo yake yaliyokumbukwa zaidi ni ushindi juu ya Mfilisti [[Goliathi]].
 
Pamoja na makosa yake, Daudi akabaki kielelezo cha mfalme wa Israeli, ambaye awe tofauti na watawala wengine wote kwa kuwa hasa mtumishi mnyenyekevu wa [[Mungu]] bila ya kuyumba kwa kuelekea [[miungu]] mingine.
 
== Habari zake katika [[Vitabu vya Samweli]] ==
Mstari 24:
Kwa [[unyenyekevu]] wake huo alimpendeza Mungu akapewa naye ahadi ya ajabu, yaani kwamba ufalme wake utadumu milele (2Sam 7). [[Utabiri]] huo wa nabii [[Nathani]] ukaja kuongoza [[tumaini]] la Waisraeli hasa walipodhulumiwa, k.mf. zamani za [[Yesu]] chini ya [[ukoloni]] wa Kirumi, ambapo wote walimtazamia [[mwana wa Daudi]] mwenye kurudisha ufalme wa Israeli.
 
Pamoja na hayo, Kishakisha kupewa ahadi hiyo alikwenda mbele ya Mungu na kusali vizuri kama kawaida yake hata nje ya ibada: [[sala]] yake ya sifa na [[shukrani]] imejaa mshangao kwa ukuu wa Mungu na [[fadhili]] zake na kumalizika kwa ombi nyenyekevu.
 
Ingawa hakukubaliwa kumjengea Mungu [[hekalu]] la ajabu alivyokusudia, amekuwa mwalimu wa sala kwa nyakati zote: hata leo [[liturujia]] ya [[Uyahudi]] na ya [[Ukristo]] inategemea sana zaburi zake.
 
Matendo mengine tofauti yaliyobadilishayaliyoathiri sana maisha ya Daudi ni [[dhambi]] alizotenda kwa ajili ya mke wa [[Uria]], yaani [[uzinifu]], [[unafiki]], [[ulevyaji]] na [[uuaji]] wa askari huyo mwadilifu (2Sam 11). Basi, [[nabii]] [[Nathani]] akamuendea ili kumlaumu na kumtabiria adhabu mbalimbali, hasa kwamba [[upanga]] hautaondoka nyumbani kwake (2Sam 12:1-25).
 
Ikawa hivyo hasa kwa sababu ya [[Absalomu]] mwanae ambaye alimuua kaka yake (2Sam 13:22-37) na baada ya kusamehewa akafanya [[njama]] hata akamfukuza Daudi toka Yerusalemu (2Sam 14:28-15:29) akazini na masuria wake mahali pa wazi (2Sam 16:20-23). Hata hivyo Daudi akazidi kumpenda na alipoambiwa ameuawa akamlilia kwa namna ambayo iliwashangaza na kuwachukiza waliompigania: lakini yeye ambaye alijiombea na kupewa [[msamaha]] wa Mungu hakumchukia mwanae aliyehatarisha maisha yake (2Sam 18:19-20:8).