TaTEDO : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 7:
==MAKAO MAKUU==
Makao yake makuu yako Dar es salaam,Tanzania.
==HISTORIA YA TaTEDO==
Mwanzo wa TaTEDO unaweza kwenda hadi miaka ya 1980 wakati mmoja wa waanzilishi wake (Nd. Estomih Sawe) alipopata nafasi ya kwenda nje ya nchi kwa masomo zaidi katika masuala ya nishati. Baada ya kurudi masomoni alifanya kazi katika Wizara ya Nishati, Madini na Maji ambapo alishiriki katika kuunda na kuendeleza kitengo cha nishati mbadala (au nishati za kujadidika).
Katika miaka ya 1985 hadi 1989, alishiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali kama mradi wa nishati wa GTZ katika mikoa ya Dar es salaam, Mafia na Kondoa. Mradi mwingine ulikuwa wa majiko na uchomaji mkaa uliofadhiliwa na Benki ya Dunia ambao ulipitishwa mwaka 1988. Katika utekelezaji wa mradi huu, wataalamu kadhaa kutoka nje ya nchi waliajiriwa akiwemo Dk. Maxwell Kinyanjui kutoka Kenya (Mtaalam wa Majiko), Ibrahim Ndiaye kutoka Senegali ( mtaalam wa uchomaji mkaa) na Rainer German(Mtaalam wa Tanuru la Nusu Chungwa). Kulikuwa na majadiliano ya mara kwa mara kati ya Nd. Sawe na Dk Kinyanjui ambayo yalikuwa yakiendelea hata baada ya saa za kazi .
Kati ya changamoto ambazo walikutana nazo wataalamu hawa ilikuwa namna ya kuweza kukifanya haya yaliyoletwa na mradi mradi kuwa endelevu. Mawazo mbalimbali yalipendekezwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha kiwanda cha uzalishaji wa majiko sanifu. Hata hivyo mawazo haya yalishindikana kutokana na kukosekana kwa wajasiriamali waliokuwa tayari kuwekeza katika biahara ya majiko sanifu
Mwaka 1989, lilijitokeza wazo la kuanzishwa kwa taasisi isiyo ya kiserikali ya nishati katika majadiliano baina ya Mr Sawe na Dk Kinyanjui. Wazo hili lilikubaliwa na wataalam hawa wawili kwa kuzingatia mafanikio ya asasi nyingine kama KENGO ya Kenya . majadiliano yaliendelea ili kupata jina la asasi. Dk Kinyanjui alipendekeza jina la Tanzania Wood Energy Non-Governmental Organization (KWENGO). Jina hilo lilikubaliwa na katiba ya mwanzo iliandaliwa kwa kutumia jina hili.
Baada ya muda Nd. Sawe aliona ni vizuri ikaanzishwa asasi ambayo itajumuisha teknolojia nyingine za kujadidika za nishatu na jina la asasi likabadilika kuwa “Tanzania Traditional Energy Organization”(TaTEDO)
xxxxxxxxxxxxxxx
Mwaka 1989 Nd Sawe alimtambulisha Dk Kinyanjui kwa Mzee Daniel Yona na Mwalimu Joshua Meena ambaye kwa wakati huo alikuwa mwalimu Mstaafu na Mzee Yona alikuwa mfanyabiashara. Wote walikubaliana na wazo hilo na wakaanza mikutano ya pamoja ya kuanzisha TaTEDO. Mkutano wa kwanza ulifanyika nyumbani kwa Mzee Yona mwaka 1990 ambao uliongelea katiba ya kwanza walioudhuria walikuwa waanzilishi wa TaTEDO Mzee Daniel Yona, Mwalimu Joshua Meena , Nd. Estomih Sawe na Dk Maxwell Kinyanjui
Katika kikao hiki katiba ya kwanza ya TaTEDO iliyoandaliwa na Mr Sawe na Dr Maxwell ilijadiliwa na kuamuliwa kusajili Asasi hii baada ya katiba kupitiwa na mwanasheria Mr Temu. Iliamuliwa pia kuongeza watu wengine ili kufuikia idadi ya watu kumi na mbili waliotakiwa kwa ajili ya usajili.
Kikao cha kwanza cha taasisi kilimteua Mzee Yona Kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa TaTEDO, Mr. Estomih Sawe kuwa makamu wa mwenyekiti, Mwalim Meena katibu wa kwanza na Dr Maxwell alipendekezwa kuwa mshauri
Waanzilishi hawa wane walichangia jumal ya Shilingi 52,000 kuwezesha usajili wa TaTEDO. mwenyekiti na katibu walipewa julumu la kusajili taasisi KWA SABABU Mr Sawe na Dr Maxwell walikuwa bado wafanyakazi wa serikali.
Mwenyekiti na katibu walifuatilia usajili ambao ulitolewa tarehe 29/5/1990 na hii ndi siku rasmi ya kuzaliwa TaTEDO.
Awamu ya kwanza
Awam ya kwanza ya TaTEDO illikumbwa na changamoto nyingi kutokana na uzoefu mdogo wa taasisi zisizo za kiserkiali wa wanzilishi wa taasisi. Awamu hii TaTEDO iliongozwa na Mwalimu Joshua Meena . Hata hivyo kwa ushiriakino na wadau mbalilmbali TaTEDO iliweza kusimama. Wanachama wa kwanza wa TaTEDO walikuwa ni mafundi wa majiko sanifu pamoja na wakulima.
Katika kipindi hiki tatedo ilifanya kazi Dar es Salaam peke yake. Katika kipindi hiki TaTEDO ilipata Ufadhili Kutoka HIVOS mwaka 1992, NORAD mwaka 1993, FINNIDA, pamoja na CIDA.
Mabadiliko ya uongozi mwaka 1997
Mwaka 1996 mwalimu Meena aliomba kupumzika na hivyo kufikia mwisho wa awamu ya kwanza. TaTEDO iliamua kutafuta mtu mwenye utaalam wa Nishati Jadidifu ili kuongeza kasi ya maendeleo ya Tassisi . Uongozi mpya chini ya Mkurugenzi wa sasa Bwana Sawe uliingia ukiwa na mikakati mipya ya kuendeleza huduma za nishati endelevu . katika kipindi hiki dhamira na maono ya Tasisi yalibadilika ambapo taasisi ilianza ,mikakati ya kuboresha uwezo wa rasilimali watu kwa kuajiri wasomi na kuendeleza waliopo. Katika kipindi hiki taasisi imeongeza uwezo wa rasilimali na kuongeza. Na kuongeza eneo la utendaji kazi kutoka mkoa mmoja wa Dar es Salaam hadi mikoa mitano ya Arusha, Pwani , Kilimanjaro , Mwanza na Shinyanga .
Pia katika kipindi hiki idadi ya wafanyakazi imeongezeka kutoka kutoka 15 mwaka 1996 hadi 56 mwaka 2010. Katika kipindi cha miaka ishirini ya TaTEDO kiasi cha fedha kinachotumika kwa mwaka kimeogezeka kutoka shilingi 54,000 mwaka 1990 hadi shilingi billion 2.9 mwaka 2009.
 
==Muundo wa Taasisi==