Ramadan (mwezi) : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 10:
 
katika quran
sura 2 aya 185, ,, Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru .
 
Kusoma Qurani
Amesema Allah (Subhaanahu wa Ta’ala);
“Mwezi wa Ramadhani ambayo imeteremshwa ndani yake Qur-an hali ya kuwa ni uongofu kwa watu …………"
Kwa kuwa katika mwezi huu ndio Qurani iliteremshwa kwa Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam), inatakiwa kwa muislam kufanya bidii kuisoma angalau juzuu moja kwa siku ili aweze kumaliza msahafu ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Ramadhan.
 
Kuharakisha kufungua
Miongoni mwa sunna tukufu zinazotakiwa kwa mfungaji katika mwezi huu kuzikimbilia, ni kuharakisha kufungua baada tu ya kuzama jua, kwani Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amesema katika hadithi iliopokewa na Tirmidhy, Ibnu khuzayma na Ibnu Habban, amesema Bwana Mtume Muhammad (Swallah Llahu alayhi wa sallam);
“Hakika nimpendaye zaidi miongoni mwa waja wangu ni anayefanya haraka katika wao kufungua saumu.”
 
Kusali usiku
Inatakiwa kwa muislam kuyatumia masiku ya mwezi huu mtukufu katika kumuabudu Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa kusali na kufanya ibada nyengine, kwani ni mwezi wa pekee ambao ndani yake kunapatikana usiku wa cheo (Laylatul Qadr) ambao ibada ya usiku huo inalingana na ibada ya miezi elfu moja, na kwa hekima yake Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) hakutubainishia kuwa ni usiku wa tarehe ngapi. Na hii ni moja miongoni mwa fadhila za kusali katika masiku ya mwezi huu. Vile vile mwenye kusimama kwa ibada katika masiku haya husamehewa makosa yake yote yaliotangulia, kama alivyosema Bwana Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam):
“Mwenye kusimama usiku wa Ramadhani kwa kufanya ibada hali ya kuwa na imani na kutaraji thawabu anasamehewa yoteyaliotangulia miongoni mwa makosa yake.”
( Bukhari na Muslim).
v Kula daku
Kula daku vile vile ni miongoni mwa sunna tukufu zinazodharauliwa na wengi kati ya waislam na fadhila zake ni kubwa kupita kiasi, miongoni mwazo ni kurehemewa na Allah na kutakiwa msamaha na malaika watukufu kama alivyosema Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) katika hadithi;
“Hakika Allah na Malaika wake wanawarehemu wenye kula daku.”
(Twabrani, Ibnu Habban).
Vile vile Bwana Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amesisitiza katika hadithi kwa kusema kuwa:
“Hakika daku ni baraka amekupeni Allah, hivyo basi musiiache”.
(Annasai)
v Kukaa Itikaaf
Inatakiwa kwa muislam kuujaalia mwezi huu na kuutumia katika kuchuma na kuvuna aina tofauti ya mema ikiwemo Itikaaf, kwani ni miongoni mwa ibada bora sana zinazomkurubisha mja kwa Mola wake (Subhaanahu wa Ta’ala) hasa awapo katika mwezi huu wa Ramadhani, kwani baadhi ya wanavyuoni wamesema kuwa haisihi ibada hii ya itikaaf pasi na funga. Na yatoshe malipo makubwa yaliotajwa katika hadithi;
Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) amesema;
“Mwenye kukaa itikaaf siku kumi katika mwezi wa Ramadhani, basi ni kama aliyehiji na akafanya umra mara mbili mbili."
(Bayhaq)
v Kutoa sadaka
Miongoni mwa ibada tukufu alizokuwa akizifanya Bwana Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ni kutoa sadaka na alilipa umuhimu sana jambo hili hadi wakati wa kuondoka kwake ulimwenguni alipokuwa katika sakaratul mauti kila alipopata fahamu ilikuwa akimuuliza Bibi Aisha (‘Alayhis Salaam) iwapo ashazitoa sadaka zile dirhamu nne zilizokuwa nyumbani? Kadhalika kutoa huku kwake kulikuwa kukiongezeka katika Ramadhani.
v Kumtaja Allah (Subhaanahu wa Ta’ala)
Katika mwezi huu wa Ramadhani kadhalika inatakiwa kwa muislam kuwa mengi ya maneno yake yawe katika kumtaja Allah (Subhaanahu wa Ta’ala), kwani ni jambo ambalo linasaidia katika kuusafisha moyo wake na kuiboresha funga yake. Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) ametuamrisha tumtaje kwa wingi katika aya nyingi za Qurani, na hii ndio ibada pekee aliyosema Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) kuwa ifanywe kwa wingi, na miongoni mwa aya hizo;
“Enyi Mlioamini mtajeni Allah kwa wingi na mumtakase yeye asubuhi na jioni.”
(Al- Ahzaab 41 na 42)
Kadhalika Mtume (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alitufundisha aina tofauti za kumtaja Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) ili tusichoke na jambo hili kwani mwanadamu ni mwepesi wa kuchoka na jambo moja tu. Vile vile akatuonyesha tofauti kubwa iliopo kati ya anayemtaja Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na asiyefanya hivyo kati hadithi aliposema;
“Mfano wa anayemtaja Allah na asiyemtaja ni mfano wa mtu aliyehai na aliyekufa.”
(Bukhari).
Haya ni baadhi ya yanayotakiwa kufanywa na muislam, hasa awapo ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, hivyo basi tujihimu katika kuyatekeleza haya tuliyoelezwa na tumuombe Allah atutakabaliye matendo yetu “Amin”.
 
KUTHIBITI KWA MWEZI WA RAMADHANI
 
Mas’ala: 1-Huzingatiwa katika kuthibiti kwa mwezi wa ramadhani na kuwajibika kufunga mwezi wa Ramadhani njia hizi zifuatazo:
 
1- Mukallaf auone mwezi yeye mwenyewe. 2- Apate yakini au matumaini kutokana na kuenea kwa habari za kuonekana kwa mwezi huo au habari zingine zithibitishazo suala hilo katika nchi yake au sehemu yenye hukumu kama hiyo.
 
3- Kupita siku thalathini za mwezi wa shaaban. 4-Kutoa ushahidi wanaume wawili waadilifu ya kuwa wameuona ( na hapo nyuma tumekwisha elezee maana ya uadilifu ) na huzingatiwa kuwa kinacho tolewa ushahidi kiwe ni kimoja, lau mmoja wao atadai ya kuwa ameuona mwezi katika upande fulani, na mwingine akadai ya kuwa ameuona upande mwingine, kwa ushahidi huo mwezi hautathibiti, kama ambavyo huzingatiwa kutokuwepo mpingaji wa ushahidi huo- hata kama kwa kuonyesha kitendo chenye hukumu kama hiyo ya kupinga- kama ikiwa kundi la watu fulani wa nchi hiyo watatoa habari za kuonekana mwezi na wakadai kuwa wameuona mwezi na miongoni mwao kukiwemo waadifu wawili, au wakatoa habari za kuonekana mwezi kundi fulani lakini hawakudai ya kuwa wameuona mwezi isipokuwa waadilifu wawili na wengine hawakuuona na miongoni mwao kukiwa na waadilifu wawili ambao ndio wanao wawakilisha katika kufahamu sehemu pekee iliyo onekana mwezi kwa kuangalia pamoja na anga kuwa safi na kutokuwepo kinacho tarajiwa kuwa ni kizuwizi cha kuuona mwezi, katika hali kama hii ushahidi wa watu wawili waadiofu hauna iitibari yoyote, isipo kuwa ikipatikana yakiini na matumaini kutokana na ushahidi wao.
 
[[Jamii:Uislamu]]