Waraka wa kwanza kwa Wakorintho : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 7:
==Mazingira==
 
Kutoka [[Korintho]] ([[Ugiriki]]) habari za kusikitisha zilimfikia [[Mtume Paulo]] akiwa [[Efeso]] (pengine [[mwaka]] [[57]]): katika [[Kanisa]] hilo ambalo alilianzisha na kulipenda sana kulikuwa na [[shaka]] kuhusu [[imani]], ma[[mafarakanofarakano]], [[upinzani]] wa [[Wakristo]] wa Kiyahudi dhidi yake, na makwazoma[[kwazo]].
 
Kilichohatarisha zaidi [[jumuia]] hiyo ni [[karama]] mbalimbali ambazo hao Wakristo wachanga walizijali mno na hatimaye wakajivunia kuwa nazo.
 
Vilevile walivutiwa kumfuata mtu kama [[Apolo]], mwenye [[ujuzi]] na [[ufasaha]] mkubwa, mambo yaliyopendwa sana na [[Wagiriki]].
 
Ilimbidi Paulo arekebishe [[hali]] hiyo ili kuokoa hasa [[umoja wa Kanisa]] na [[heshima]] kwa viongozi wake halali.
 
Basi mwaka mzima akawa na mahangaiko kwa wafuasi wake wa Korintho akawaandikia walau barua nne au tano, ingawa sisi tunazo mbili tu; pengine sehemu za baadhi yake zimeshonwa ndani ya 2Kor.