Katerina wa Siena : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d r2.7.2) (Roboti: Imeongeza lb:Catherine vu Siena
No edit summary
Mstari 43:
 
== Utukufu ==
 
Katerina da Siena alitangazwa na [[Papa Pius II]] kuwa mtakatifu mwaka [[1461]].
[[Papa Paulo VI]] alimtangaza [[mwalimu wa Kanisa]] tarehe [[4 Oktoba]] [[1970]].
 
==Sala zake==
Mungu wa milele, Utatu wa milele,
umefanya damu ya Kristo iwe azizi kabisa kwa kushiriki umungu wako.
 
Wewe ni fumbo la kina kuliko bahari;
kadiri ninavyotafuta naona; na kadiri ninavyoona nakutafuta.
 
Siwezi kamwe kushiba; ninachopokea kitanifanya daima nitamani zaidi.
 
Unapojaza roho yangu nazidi kuonea njaa na shauku mwanga wako.
 
Hasa natamani kukuona wewe, mwanga halisi, jinsi ulivyo.
 
Ndiwe muumba wangu, Utatu wa milele, nami ni kiumbe chako.
 
Umenifanya kiumbe kipya katika damu ya Mwanao,
nami najua unavutwa na uzuri wa kiumbe chako kutokana na upendo.
 
 
Bwana wangu, elekeza jicho la huruma yako juu ya taifa lako
na juu ya mwili wa fumbo wa Kanisa takatifu.
 
Wewe utatukuzwa zaidi sana kwa kusamehe na kuwaangazia akili wengi,
kuliko kwa kupokea heshima toka kwa kiumbe mmoja duni,
kama nilivyo mimi, ambaye nilikukosea sana
na kuwa sababu na chombo cha maovu mengi.
 
Ingenitokea nini kama ningeona mimi ni hai, na watu wako wamekufa?
 
Ingekuwaje kama ningeliona gizani,
kutokana na dhambi zangu na za viumbe wengine,
Kanisa lako, Bibiarusi wako mpenzi, lililozaliwa liwe mwanga?
 
Basi, nakuomba huruma kwa taifa lako
kwa ajili ya ya upendo usioumbwa uliokusukuma wewe
umuumbe mtu kwa sura na mfano wako.
 
Sababu gani ilikufanya umweke mtu katika heshima kubwa hivyo?
 
Bila ya shaka ni upendo ule usiothaminika ambao
ulimuangalia kiumbe chako ndani mwako ukachanganyikiwa naye.
 
Lakini baadaye kwa dhambi aliyoitenda akapoteza ukuu huo uliomuinulia.
 
Ukisukumwa na moto huohuo ambao ulituumba,
ulipenda kuwatolea binadamu njia ya kupatanishwa nawe.
 
Ndiyo sababu umetupatia Neno, Mwanao pekee.
 
Amekuwa mshenga kati yako na sisi,
amekuwa haki yetu aliyeadhibu ndani mwake maovu yetu.
 
Alitii agizo ambalo wewe, Baba wa milele, ulimpa ulipomvika utu wetu.
 
Lo, kilindi cha upendo! Moyo upi hautajaa mhemko kwa kuona ukuu huo
kushukia unyonge mkubwa kama huu, yaani ubinadamu wetu?
 
Sisi ni mfano wako, nawe mfano wetu
kutokana na muungano uliouanzisha kati yako na binadamu,
ukifunika umungu wa milele
kwa wingu maskini la utu ulioharibika wa Adamu.
 
Kwa sababu gani? Bila ya shaka kwa upendo.
 
Kwa upendo huo usiosemeka nakuomba na kukuhimiza
uwawie huruma viumbe wako.
 
== Maandishi ==