Roberto Bellarmino : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d r2.6.3) (roboti Nyongeza: hr:Robert Bellarmino
No edit summary
Mstari 36:
 
Miaka ya mwisho alitunga [[katekisimu]] (kubwa na ndogo) iliyoenea sana hadi mwisho wa [[karne ya 19]].
 
==Sala yake==
 
Wewe, Bwana, u mwema, umekuwa tayari kusamehe,
na mwingi wa fadhili, kwa watu wote wakuitao;
nani hatakutumikia kwa moyo wote baada ya kuanza kuonja walau kidogo
utamu wa mamlaka yako ya Kibaba?
 
Unawaagiza nini watumishi wako, Bwana?
 
Unasema, Jitieni nira yangu. Na nira yako ikoje?
 
Unasema, Nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
 
Nani hatabeba kwa moyo radhi kabisa nira isiyobana bali inapendeza,
na mzigo usiolemea, bali unainua?
 
Kwa hiyo umeongeza kwa haki, Nanyi mtapata raha nafsini mwenu.
 
Na ikoje nira yako hiyo ambayo haichoshi, bali inapumzisha?
 
Kwa hakika ndiyo amri ya kwanza tena kuu,
Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote.
 
Nini ni rahisi, nono na tamu kuliko kupenda wema, uzuri na upendo?
 
Na hayo yote ndiwe wewe, Bwana Mungu wangu.
 
Nawe unafikia hatua ya kuahidi tuzo kwa wale wanaoshika sheria zako,
ingawa tayari zenyewe ni za thamani kuliko dhahabu nyingi,
na tamu kuliko sega la asali?
 
Ndiyo, unaahidi kweli tuzo, tena tuzo kubwa mno.
 
== Maandishi ==
[[Picha:Roma-santignazio2.jpg|thumb|right|350px|Kaburi la Roberto Bellarmino ndani ya [[Kanisa la Mt. Ignas wa Loyola kwenye Campo Marzio]] huko Roma]]